Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia... Madrid na Pachuca, Juve na Wydad

CWC Pict

Muktasari:

  • Mbappe alikosa mechi ya kwanza ya Real Madrid dhidi ya Al-Hilal, iliyomalizika kwa sare ya 1-1, kutokana na kuumwa na kulazimika kupelekwa hospitali.

LOS ANGELES, MAREKANI: REAL Madrid itashuka uwanjani bila ya huduma ya supastaa wao Kylian Mbappe katika mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Pachuca, Jumapili.

Mbappe alikosa mechi ya kwanza ya Real Madrid dhidi ya Al-Hilal, iliyomalizika kwa sare ya 1-1, kutokana na kuumwa na kulazimika kupelekwa hospitali.

Fowadi huyo Mfaransa ameshatoka hospitali, lakini haonekani kuwa fiti kwa ajili ya mechi hiyo. Beki wa kati Antonio Rudiger anaweza kurejea kwenye kikosi kwenye mechi hiyo ya wikiendi, lakini bado kuna mashaka makubwa juu ya Dani Carvajal, David Alaba, Eder Militao na Eduardo Camavinga, ambao wamekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeraha makubwa.

Ferland Mendy na Endrick nao hawamo kwenye kikosi, ambapo walibaki Hispania kuendelea na matibabu wakisubiri kuwa fiti kwa ajili ya msimu wa 2025-26. Mastaa wapya, Trent Alexander-Arnold na Dean Huijsen walicheza mechi ya kwanza dhidi ya Al-Hilal na wawili hao wanatazamiwa kuanza katika mchezo huo.

Kocha mkuu wa Real Madrid, Xabi Alonso huenda akaanza na kikosi kisichokuwa na mabadiliko yoyote, ikiwamo nafasi ya kiungo Gonzalo Garcia, ambaye alifunga bao kwenye mechi ya Al-Hilal.

Pachuka itaingia uwanjani kusaka ushindi wake wa kwanza baada kupotez amechi ya kwanza kwa mabao 2-1 dhidi ya FC Salzburg, ambao ndio vinara wa Kundi H.

Mechi nyingine za mikikmikiki hiyo ya Kombe la Dunia la Klabu itakayopigwa Jumapili ni ile ya Juventus dhidi ya Wydad Casablanca. Mechi hiyo ya Kundi B itakuwa ya pili kwa kila timu, huku Juventus ikisaka ushindi wa pili ili kujihakikishia nafasi ya kutinga raundi inayofuata, huku Wydad inayotumikiwa na Mtanzania, Seleman Mwalimu itajaribu kupambana kuandikisha ushindi wao wa kwanza baada ya kupoteza mbele ya Manchester City katika mchezo wa kwanza.

Mechi zilizochezwa usiku wa kuamkia Jumapili, River Plate ilikuwa na shughuli mbele ya Monterrey kwenye Kundi E, wakati Fluminense ilimaliza ubishi na Ulsan Hyundai katika Kundi F.