Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kombe la Dunia kuwa na 'half-time show'

SHAKIRA Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa FIFA, onyesho hilo la mapumziko litakuwa sehemu ya kuendeleza mapinduzi ya burudani katika soka huku likilenga kuongeza mvuto wa kimataifa wa fainali hiyo na pia kusaidia miradi ya kijamii kupitia mfuko maalum wa “FIFA Global Citizen Education Fund.”

NEW JERSEY, MAREKANI: SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limetangaza mpango wa kuwa na onyesho la mapumziko (halftime show) kwa mara ya kwanza kabisa katika fainali ya Kombe la Dunia 2026, litakalofanyika katika Uwanja wa MetLife, New Jersey, Marekani.

Katika tukio hilo linatarajiwa kuvuta mamilioni ya watazamaji duniani, mastaa wakubwa wa muziki akiwemo Shakira, Madonna na kundi maarufu la K-pop BTS wanatajwa kuwa sehemu ya burudani hiyo kubwa itakayoratibiwa na kiongozi wa Coldplay, Chris Martin.

SHAKI 01

Kwa mujibu wa FIFA, onyesho hilo la mapumziko litakuwa sehemu ya kuendeleza mapinduzi ya burudani katika soka huku likilenga kuongeza mvuto wa kimataifa wa fainali hiyo na pia kusaidia miradi ya kijamii kupitia mfuko maalum wa “FIFA Global Citizen Education Fund.”

Mfuko huo unalenga kusaidia kuboresha upatikanaji wa elimu bora na maendeleo ya mpira wa miguu kwa watoto duniani, hasa katika maeneo yenye changamoto za kijamii na kiuchumi.

Shakira anatarajiwa kuwa mmoja wa nyota wa tukio hilo, pia ameripotiwa kuandaa wimbo rasmi wa Kombe la Dunia uitwao “Dai Dai”, ambao utazinduliwa siku ya ufunguzi wa Kombe la Dunia.

SHAKI 02

FIFA imesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuifanya fainali ya Kombe la Dunia kuwa tukio la burudani la kiwango cha juu zaidi duniani, likiunganisha michezo, muziki na utamaduni kwa wakati mmoja.

Mashindano ya Kombe la Dunia 2026 yatashuhudia zaidi ya mechi 100 katika miji 16 ya Marekani, Canada na Mexico na yataanza rasmi Juni 11 huku mataifa 48 yakishiriki kwa mara ya kwanza katika historia.

SHAKI 03

Mbali na fainali, FIFA pia imepanga sherehe kubwa za ufunguzi katika miji mbalimbali ya wenyeji ambapo wasanii kama Katy Perry, Future, Anitta, LISA na wengine wengi watatumbuiza.