Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shakira azama katika penzi zito

SHAKIRA Pict

Muktasari:

  • Shakira aliyetamba na viabo kama ‘Hips dont Lie’, ‘This time for Africa’ na nyinginezo baada ya kuachana na baba watoto wake beki wa Barcelona, Gerald Pique utengano ulikokuwa gumzo duniani.

KUNA tetesi zinazoendelea mitandanoni, staa wa muziki wa Pop duniani, Shakira yupo kwenye uhusiano  mpya wa kimapenzi na muigizaji wa Uingereza, Lucien Laviscount.

Inaelezwa chanzo cha ukaribu wao ni walipokutana wakati wa kurekodi video ya wimbo mwaka 2024. Kwenye skrini walikuwa na kolabo nzuri na baadhi ya mashabiki walianza kutilia shaka je ni ugizaji tu au kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia.

Muda mfupi baadaye, walionekana wakila chakula cha usiku pamoja jijini New York, jambo lililoongeza moto kwenye uvumi huo.

Sasa shida sio uhusiano wao kinachoongelewa zaidi ni gepu la umri baina ya wawili hao Shakira akiwa na miaka 48 wakati Lucien ana 30 tofauti ya zaidi ya miaka 10.

Wengine wanadai muigizaji huyo amefuata pesa kwa Shakira ambaye anajinyakulia mamilioni ya pesa kutokana na kazi zake za muziki.

Licha ya kelele hizo hadi sasa hakuna mmoja wao aliyezungumza kuhusu uhusiano wao licha ya kuendelea kuonekana sehemu tofauti wakiwa pamoja.

Shakira aliyetamba na viabo kama ‘Hips dont Lie’, ‘This time for Africa’ na nyinginezo baada ya kuachana na baba watoto wake beki wa Barcelona, Gerald Pique utengano ulikokuwa gumzo duniani.