KOMBE LA DUNIA: England wapambanaji wenye ndoto isiyotimia

DOHA, QATAR. ENGLAND ni miongoni mwa timu nane ambazo zmewahi kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia. England ilibeba ubingwa 1966 na sasa inashiriki fainali hizo ikisaka ubingwa wa pili.

Vilevile ilimaliza katika nafasi ya nne mara mbili katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika 1990 na 2018. Englad ina udhaifu mkubwa katika changamoto ya mikwaju ya penalti katika fainali za Kombe la Dunia kwani iliwahi kuboronga hatua ya makundi katika michuano tofauti.

England iltinga nusu fainali ya Kombe la Dunia 2018, lakini ikafungwa mabao 2-1 ilipocheza dhidi ya Croatia. Vilevile ilishinda kutoboa katika kinyang’anyiro cha kusaka mshindi wa tatu na kupoteza ilipocheza dhidi ya Ubelgiji.

Licha ya kusuasua katika michuano ya Nations League mwaka huu England inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na kikosi chake ambacho kinapondwa na baadhi ya wadau wa soka nchini humo kwamba hakitatoboa Qatar.


KWA NINI ENGLAND?

Licha ya kusuasua England ina wachezaji wapambanaji ambao wamekiwasha Ligi Kuu England misimu tofauti kama Harry Kane, Jack Grealish, Raheem Sterling, Marcus Rashford na Bukayo Saka wanaounda kikosi cha kocha Gareth Southagate kuelekea fainali za Kombe la Dunia Qatar.

Mastaa hao wana ndoto ya kubeba Kombe la Dunia kwani wamepania kufanya vizuri.

Kane anategemewa katika safu ya ushambuliaji kutokana na ubora wake wa kupachika mabao na ikumbukwe straika huyo ni mfungaji bora wa Tottenham Hotspur wa muda wote. Straika anayekipiga Manchester United, Marcus Rashford anapewa nafasi na Southgate baada ya kumshawishi katika ligi, hivyo anatarajiwa kuona kiwango chake akikihamishia Qatar. Licha ya kupondwa msimu wake wa kwanza alipojiunga na Manchester United, lakini Southgate amekuwa akiamini uwezo wake sambamba na Bukayo Saka anayekipiga Arsenal. Hata hivyo, licha ya kusuasua Reaheem Sterling msimu huu katika chama lake jipya la Chelsea alikotua akitokea Manchester City, nyota huyo ni mongoni mwa mastaa wanaotegemewa kutokana na kasi yake anapokuwa eneo la hatari, hivyo anategemewa kuwa mwiba langoni mwa wapinzani wao akishirikiana na washambuliaji wengine.