KOMBE LA DUNIA 2022: Ujerumani vigogo wenye kiu ya mafanikio

DOHA, QATAR. UJERUMANI ndio timu iliyopata mafanikio makubwa katika mashindano ya kimataifa. Imebeba ubingwa wa Kombe la Dunia mara nne. Ubingwa wa kwanza wa Kombe la Dunia ilichukua mwaka 1954.

Baada ya hapo Ujerumani ikaanza kuwa na uzoefu wa fainali na kutwaa tena kombe hili mwaka 1974, 1990 na mwaka 2014 katika mashindano yaliyofanyika Russia.

Mwaka 2018 haukuwa mzuri kwa Ujerumani. Ilifuzu hatua ya makunda ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja. Ilishirki fainali hizo ikwia ni bingwa mtetezi lakini ikaangukia pua raundi ya 16 bora.

Ujerumani iliwakosa wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza kama kama kina Marco Reus nafasi yake ilichukuliwa na Leroy Sane, kipa wao tegemeo Manuel Neuer aliyekosa fainali hizo dakika za mwisho baada ya kuumia.


KWA NINI

UJERUMANI?

Ujerumani inashiriki tena fainali za Kombe la Dunia huku Qatar ikipewa nafasi ya kufanya maajabu kutokana na kikosi chake kilichosheheni wachezaji hatari wanaocheza ligi mbalimbali.

Neuer ni kipa tegemeo anayetegemewa katika kikosi kutokana na uzoefu wake. Amecheza fainali mbili za Kombe la Dunia kuanzia mwaka 2014 na 2018. Aliiongoza Ujerumani kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia katika fainali zilizofanyika Brazil, mwaka 2014. Straika Thomas Muller licha ya kutofunga bao katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Russia bado ni mchezaji tegemeo mwenye uzoefu.

Fowadi huyo anayekipiga Bayern Munich anaichukia michuano ya Euro kwasababu hakuwahi kufunga bao ilivyofanyika mwaka 2012.

Mwigine nyota wa Chelsea, Kai Harvetz pamoja na Joshua Kimmich.Jamal Musiala anashiriki fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia soka lake, kinda huyo amekuwa hatari katika kikosi cha Bayen Munich msimu huu anayesubiriwa kwa hamu na mashabiki wakione kipaji akiwa na uzi wa Ujerumani. Bila kumsahau Antonio Rudiger anayekipiga Real Madrid ni miongoni mwa mabeki hodari na tegemeo ndani ya kikos hicho ambao wapo tayari kukiwasha Qatar. Ujerumani mara nyingi hutumia mfumo wa 4-2-3-1.