Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa ndondi atamani kumsaidia Cristiano Ronaldo kiakili

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Scott ambaye Septemba 2024 alifunga ndoa na mtangazaji maarufu wa CBS Sports, Kate Abdo, ameweka wazi mpango huo akimaanisha hitaji lake la kumsaidia Ronaldo ambaye bado anapendwa na mashabiki wake ulimwenguni kote.

Kocha wa masumbwi, Malik Scott, ameweka wazi namna anavyoweza kumsaidia mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, kuboresha hali yake ya kiakili katika hatua hii ya mwisho ya taaluma yake.

Scott ambaye Septemba 2024 alifunga ndoa na mtangazaji maarufu wa CBS Sports, Kate Abdo, ameweka wazi mpango huo akimaanisha hitaji lake la kumsaidia Ronaldo ambaye bado anapendwa na mashabiki wake ulimwenguni kote.

Akiwa katika mahojiano na Canada Casino, kocha huyo mwenye umri wa miaka 44, amesema angefurahi kufanya mazungumzo ya kina na Ronaldo kuhusu maisha ya ushindani wa kiwango cha juu. 

Ameongeza kuwa anafahamu changamoto za kiakili zinazowakumba wanamichezo wa kiwango cha dunia, na anaamini anaweza kuongeza kitu kwenye uwezo wa kiakili wa Ronaldo.

"Ningefurahi sana kukaa na kuzungumza na Cristiano Ronaldo kuhusu ushindani na kuongeza kitu kwenye upande wake wa kiakili. Inaweza kuwa ni mazungumzo tu ya kawaida kuhusu kile tunachoshirikiana nacho ni ushindani.

RONA 01

"Watu hawa wanajua hisia za kushindana mbele ya maelfu ya mashabiki. Kuna presha kubwa inayokuja na hilo. Mimi ni mtu ninayeielewa, bila kujali wanavyotabasamu au kucheza vizuri, bado kuna mambo wanapitia. Tunaweza kuzungumza kuhusu hayo," amesema.

Scott, ambaye alikuwa bondia wa kiwango cha juu kabla ya kustaafu, sasa ni kocha na amefanya kazi na mabondia wakubwa kama Deontay Wilder. 

Uzoefu wake wa kushindana katika mazingira yenye presha kubwa ndiyo msingi wa kile anachotaka kushirikiana na Ronaldo, ambaye anaendelea kuwashangaza mashabiki wake kwa uwezo wa kupmbana licha ya kuwa na umri mkubwa.

Mshindi huyo wa Ballon d’Or mara tano, anaendelea kuonyesha kiwango cha juu akiwa na umri wa miaka 40, na bado ni mchezaji wa kutumainiwa wa klabu ya Al-Nassr nchini Saudi Arabia, ambako anatarajiwa kumalizia soka lake akiwa huko.

RONA 03

Ronaldo anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji wa kandanda wenye nguvu kubwa ya akili, kwa jinsi anavyoweza kuonesha kiwango bora kwa muda mrefu na katika mazingira ya shinikizo kutoka kwa wachezaji na mashabiki wa timu pinzani. 

Licha ya umri wake, bado ana nia ya kuipeleka timu ya taifa ya Ureno kwenye fainali za Kombe la Dunia litakalofanyika Marekani majira ya joto mwaka ujao (2026).

Scott anasema ana heshima kubwa kwa juhudi za Ronaldo kuendelea kuwa bora, na kwamba mazungumzo yao yangekuwa ya maana, si tu kwa mchezaji huyo, bali pia kwa wanamichezo wengine wanaopitia safari kama yake.