Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo aandaliwa ulinzi maalum India

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo ya hatua ya makundi, imepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Jawaharlal Nehru huko Goa, Oktoba 22, 2025.

POLISI wa Goa huko India wametoa taarifa kuhusu mipango ya usalama iwapo Cristiano Ronaldo atasafiri na klabu yake ya Al-Nassr kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Asia dhidi ya FC Goa.

Mechi hiyo ya hatua ya makundi, imepangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Jawaharlal Nehru huko Goa, Oktoba 22, 2025.

Ronaldo hakusafiri na kikosi cha Al-Nassr kilipokwenda Iraq wiki hii kwa ajili ya mechi za michuano hiyo dhidi ya Al Zawraa.

Kabla ya hapo, mshambuliaji huyo wa Ureno, hakucheza kwenye mechi dhidi ya FC Istiklol ya Tajikistan iliyopigwa Saudi Arabia.

Hata hivyo, FC Goa pamoja na Polisi wa Goa hawataki kuchukulia jambo hili kimzaha na tayari wameanza maandalizi kuhakikisha ulinzi wa hali ya juu endapo Ronaldo atasafiri na Al-Nassr hadi mjini Goa, India.

RONA 01

Mapema wiki hii, uongozi wa klabu hiyo ulikutana na polisi na Serikali ya Jimbo la Goa kujadili hatua za kiusalama iwapo Ronaldo atasafiri.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Jimbo la Goa Kusini, Tikam Singh Verma, amesema: “Mpaka sasa hakuna uthibitisho kama Ronaldo atawasili, hivyo hatuwezi kupanga ulinzi rasmi. Lakini hata tukipata taarifa ya ghafla, tunaweza kulisimamia hilo. 

RONA 02

"Tulikuwa na kikao na FC Goa na tumeamua kuongeza idadi ya askari kwa ajili ya mechi hiyo. Ikiwa Ronaldo atakuja Goa, taratibu za serikali ya jimbo na idara za usalama zitahusika pamoja na polisi wa wilaya kutoa msaada wa ziada.”

Kwa sasa mashabiki wa FC Goa, wanasubiri kwa hamu kuona kama nyota huyo wa Ureno atakuwa sehemu ya kikosi cha Al-Nassr kitakachosafiri kwenda India.