Kocha wa Aziz aachia ngazi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

WAKATI kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz KI akirejea kazini klabuni kwake kuendelea na mbio za msimu huu, kule kwao alikotoka kocha wake wa timu ya taifa, Hubert Vellud ameshtua kwa kuachia ngazi.

Vellud amesitisha mkataba mwenyewe wa kuendelea kuifundisha Burkina faso baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka miwili akiwa na wakati mzuri.

Kocha huyo amewasilisha barua ya kuachia ngazi uamuzi ambao umewashtua viongozi wa shirikisho la Soka Burkina faso huku mwenyewe akiaga rasmi kwa barua ya kwenda kwa mashabiki wa soka nchini humo.

Mfaransa huyo ameiacha Burkinabe baada ya kuifikisha hatua ya 16 ya Fainali za Mataifa ya Afrika ikitolewa na Mali kwa kupoteza kwa mabao 2-1.

Vellud ndiye kocha aliyempa nafasi kubwa Aziz KI kwenye kikosi cha timu ya taifa hilo na kwenye mechi za Afcon alimpa nafasi ya kucheza mechi tatu kati ya nne.

"Nafikiri imekuwa miaka miwili yenye mafanikio ndani ya taifa hili kubwa, naona wakati umefika niishie hapa, hatukufikia malengo yetu ya kucheza robo fainali lakini kuifanya nchi hii kuwa na timu ya taifa yenye ushindani sio kitu kidogo, nawashukuru, wachezaji, viongozi wa soka, serikali lakini kwa muhimu mkubwa mashabiki wa taifa hili," amesema Vellud.

Kwenye fainali hizo za Afcon, kocha huyo aliiongoza Burkinabe kuanzia hatua ya makundi na ilikuwa kundi d pamoja na timu za Angola, Mauritania na Algeria na ilianza na Mouritani na kuichapa bao 1-0, kabla ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Algeria na kufungwa mabao 2-0 na Angola.

Hata hivyo, Burkina Faso ilitinga hatua ya 16 bora na kukutana na Mali na kuondolewa kwa kichapo cha mabao 2-1.