Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Super Eagles atabiri bingwa wa AFCON 2025

BINGWA Pict

Muktasari:

  • Bingwa wa mwisho ni Ivory Coast, iliyotwaa ubingwa wa AFCON 2023 baada ya mashindano hayo kufanyika mwaka 2024, hivyo kuendeleza historia ya mashindano hayo yenye ushindani mkubwa barani Afrika.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Philippe Troussier, ametaja timu nane anazoamini zina uwezo wa kutwaa ubingwa wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), zilizoanza jana Jumapili Desemba 21, 2025 nchini Morocco.

Troussier ambaye alikiongoza kikosi cha Nigeria mwaka 1997, amesema ana uhakika kuwa fainali za mwaka huu zitakuwa na ushindani mkubwa na viwango vya hali ya juu, akizitaja Morocco, Ivory Coast, Senegal, Algeria, Afrika Kusini, Cameroon, Nigeria na Misri kuwa miongoni mwa timu zenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

“Nina imani kuwa fainali za AFCON 2025 zitakuwa imara na zenye ushindani mkubwa, kwangu mimi nafasi ya kwanza ninaipa Morocco ikifuatiwa na Ivory Coast, Senegal, Algeria, Afrika Kusini, Cameroon, Nigeria na Misri,” amesema Troussier.

Troussier, mwenye umri wa miaka 70, ana uzoefu mkubwa barani Afrika, akiwa amewahi kuinoa timu ya taifa ya Morocco, Burkina Faso, Ivory Coast, Nigeria na Afrika Kusini, jambo linaloipa kauli yake uzito mkubwa.

Wenyeji Morocco walianza vyema kampeni yao ya AFCON 2025 kwa kuifunga Comoros mabao 2–0 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa jana Jumapili usiku, hivyo kuimarisha nafasi yao kama taifa linalopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

KOCHA Pict

Hata hivyo, bado haijulikani kama utabiri wa Troussier utatimia, hasa ikizingatiwa kuwa Ivory Coast ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo, baada ya kutwaa taji katika fainali za 2023 zilizounguruma nchini kwao.

Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zimekuwa zikishuhudia mabingwa mbalimbali tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957. 

Misri ndiyo taifa lililotwaa ubingwa mara nyingi zaidi, likinyakua taji hilo mara saba, likifuatiwa na Cameroon yenye mataji matano na Ghana manne. Mataifa mengine yaliyowahi kutwaa ubingwa ni Nigeria (3), Ivory Coast (3), Algeria (2), DR Congo (2), Zambia, Tunisia, Sudan, Ethiopia, Morocco, Afrika Kusini, na Senegal, kila moja likitwaa taji mara moja au zaidi. 

Bingwa wa mwisho ni Ivory Coast, iliyotwaa ubingwa wa AFCON 2023 baada ya mashindano hayo kufanyika mwaka 2024, hivyo kuendeleza historia ya mashindano hayo yenye ushindani mkubwa barani Afrika.