Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona yamgeukia Lewandowski

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mkataba wa sasa wa Lewandowski unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na uongozi wa Barcelona unaamini kwamba bado supastaa huyo ana mchango mkubwa kikosini licha ya umri wake kuwa mkubwa.

BARCELONA inataka kumpa mkataba mpya wa msimu mmoja mshambuliaji mkongwe wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski, 37, lakini kwa mshahara utakaokuwa pungufu ya ule anaokunja kwa sasa.

Mkataba wa sasa wa Lewandowski unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na uongozi wa Barcelona unaamini kwamba bado supastaa huyo ana mchango mkubwa kikosini licha ya umri wake kuwa mkubwa.

Awali. ilidaiwa kuwa fundi huyo ataachwa badaa ya mkataba wake kumalizika kwa ajili ya kumpa Marcus Rashford nafasi ya kusaini mkataba wa moja kwa moja wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kwamba Barcelona imebadilisha mawazo na ipo tayari kuendelea kusalia na Lewandowski hadi mkataba wake utakapomalizika.

Tangu kuanza kwa msimu huu Lewandowski amecheza mechi 27 za michuano yote akifunga mabao 12 na kutoa asisti tatu.

Timu kibao kutoka Saudi Arabia na Marekani zimekuwa zikimnyemelea mshambuliaji huyo kwa ajili ya kupata saini yake kama mchezaji huru.

Barca inataka kuwauza baadhi ya wachezaji na kubana matumizi kiasi cha kuhakikisha inambakisha Rashrod pamoja na kumpa mkataba mpya Lewandowski.


Scott McTominay

NAPOLI ipo tayari kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na kiungo wa kimataifa wa Scotland, Scott McTominay, 29, ili aendelee kuitumikia hadi 2030.

Kwa sasa McTominay ana mkataba unaomalizika 2028, lakini uongozi unaona mchango wake kuwa mkubwa katika safu ya kiungo, hivyo unataka kumpa mkataba wa muda mrefu zaidi.

Mazungumzo yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni huku McTominay mwenyewe anaonekana kuwa na uhitaji wa kubaki.


Jhon Duran

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Colombia, Jhon Duran, 22, anatarajiwa kujiunga na Zenit St Petersburg ya Urusi kwa mkopo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuachana na Fenerbahce anayoitumikia kwa sasa kwa mkopo wa msimu mzima.

Duran anataka muda zaidi wa kucheza mara kwa mara, na Zenit inaonekana kuwa tayari kumpa nafasi hiyo ili kurejesha makali yake kutokana na kipindi kigumu anachopitia nchini Uturuki.


Sandro Tonali

JUVENTUS imemuweka kiungo wa Newcastle United na timu ya taifa ya Italia, Sandro Tonali, 25, katika orodha ya wachezaji inaotamani kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mabingwa hao wa zamani wa Serie A wanaonekana kuwa tayari kufanya kila linalowezekana kumrudisha Tonali Italia wakiamini uzoefu wake Ligi Kuu England utaongeza ubora na ushindani katika safu yao ya kiungo.


Cristiano Ronaldo

HATIMA ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, 41, ndani ya klabu ya Al-Nassr ipo shakani na baadhi ya timu zinafikiria kuvunja mkataba wake ambao una kipengele kinachoeleza anaweza akauzwa kwa Pauni 44 milioni.

Licha ya umri wake, Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji wenye ushawishi ndani na nje ya uwanja. Timu nyingi zinaamini jina lake lina faida kubwa kibiashara.


Jesse Lingard

FEYENOORD ni miongoni mwa timu zinazofanya mawasiliano na wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa England, Jesse Lingard, 33, ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kuachana na FC Seoul.

Kocha wa Feyenoord, Robin van Persie aliwahi kucheza na Lingard Manchester United, na sasa anadaiwa kuwa ndiye alipendekeza jina lake akiamini atasaidia kikosini. Lingard anataka kupata changamoto mpya barani Ulaya.


Alejo Veliz

MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspur na Argentina, Alejo Veliz, 22, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Rosario Central anatarajiwa kujiunga na Bahia ya Brazil katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya Euro 9 milioni pamoja na nyongeza ya zaidi ya Euro 3 milioni. Vigogo wa Spurs wapo tayari kumruhusu staa huyo kuondoka.


Gabri Veiga

ATLETICO Madrid imekuwa ikionyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa FC Porto na timu ya taifa ya Hispania, Gabri Veiga, 23, na dili la karibuni limefeli siku ya mwisho ya dirisha la usajili la majira ya baridi.

Porto ilikataa ofa na ikasisitiza kuwa Veiga bado ni sehemu muhimu ya mipango ya msimu huu.

Veiga amekuwa akionyesha kiwango kizuri na uwezo mkubwa wa kutengeneza mashambulizi.