Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Spurs ataja siri ya kichapo cha Arsenal

SPURS Pict

Muktasari:

  • Kiungo mshambuliaji wa England, Eberechi Eze alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ akitanguliwa na kiungo mwenzake kutoka Ubelgiji Leandro Trossard  aliyefunga bao la kwanza, huku   Richarlison akiifungia Spurs bao la kufutia machozi.

Kocha wa Tottenham Hotspurs, Thomas Frank, amekiri kikosi hicho kilicheza chini ya kiwango, hali iliyosababisha kupoteza mechi ya Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Arsenal iliyoibuka na ushindi wa 4-1, jana Jumapili, Novemba 23, 2025.

Kiungo mshambuliaji wa England, Eberechi Eze alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ akitanguliwa na kiungo mwenzake kutoka Ubelgiji Leandro Trossard  aliyefunga bao la kwanza, huku   Richarlison akiifungia Spurs bao la kufutia machozi.

Kocha Frank, ameiambia Sky Sports kuwa, kikosi hicho cha Coys kilicheza tofauti au maelekezo yake, tena chini ya kiwango ambacho hakukitarajia, hivyo kilichotokea baada ya dakika 90 kilistahili kutokea.

Kocha huyo raia wa Denmark, amesema matokeo hayo yamemuuza sana, kutokana na maandalizi makubwa aliyoyafanya kabla ya mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Emirates, lakini amesisitiza kurekebisha upungufu aliouona kabla ya kuikabili Fulham mwishoni mwa wiki hii.

SPU 01

“Kikosi changu hakikucheza vizuri, wachezaji walicheza tofauti na maelekezo niliyowapa, kwa hakika inaumiza sana, kwani tulijiandaa vizuri na matumaini yalikuwa makubwa sana kabla ya kuja hapa (Emirates), lakini kilichotokea hatuna budi kukipokea.”

“Nadhani bila kujali kama timu zote mbili zilijaribu kucheza kwa pasi fupi, wao walipata faida zaidi na sisi hatukuweza kutoka.”

“Timu ilipotumia mipira mirefu, hatukufanikiwa vya kutosha. Mfano ni bao la pili na la tatu, ambapo mchezaji mmoja alipenya kati ya wachezaji wawili au watatu. Utendaji mbaya na tumepoteza.”
 “Tunarudi kwenye uwanja wa mazoezi, nitajitahidi kurekebisha upungufu ulioonekana katika mechi ya jana dhidi ya Arsenal. Ninaipongeza The Gunners kwa mechi nzuri ambayo imeisha kwa furaha upande wao.”

SPU 02

“Lingine niwaombe radhi mashabiki wetu, ambao walikuwa pamoja nasi wakati wote, kwa hakika tutakuwa tumewakwaza kwa matokeo haya, lakini ninawasihi waendelee kuwa na sisi katika mapambano ya kuendelea kusaka pointi katika Ligi Kuu na michuano mingine inayotukabili msimu huu.” Amesema kocha huyo mwenye miaka 52

Arsenal imefikisha pointi 29 ikiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi ya EPL, kwa tofauti ya pointi 6 dhidi ya Chelsea inayokamata nafasi ya pili baada ya mechi za raundi ya 12, huku Spurs ikisalia nafasi ya 9 kwa kuwa na pointi 18 baada ya mechi 12.