Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Spurs afunguka ishu ya Man United

SPURS Pict

Muktasari:

  • Wakati Kocha Erik ten Hag alipokuwa akijiandaa kwa mechi hiyo dhidi ya Manchester City uwanjani Wembley, mmiliki mwenza wa Man United, bilionea Ratcliffe alifanya mazungumzo na kocha Frank kwenye maegesho yake huko London.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Thomas Frank amefunguka kwamba alifanyiwa usaili na bosi wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe kwa ajili ya kwenda kuinoa timu hiyo siku moja kabla ya kubeba taji la Kombe la FA  mwaka 2024.

Wakati Kocha Erik ten Hag alipokuwa akijiandaa kwa mechi hiyo dhidi ya Manchester City uwanjani Wembley, mmiliki mwenza wa Man United, bilionea Ratcliffe alifanya mazungumzo na kocha Frank kwenye maegesho yake huko London.

Man United ilizungumza na makocha kadhaa mwishoni mwa msimu wa 2023-24 wakati ilipokuwa ikitafuta kocha mpya kabla ya kumfuta kazi Ten

Thomas Tuchel, Roberto De Zerbi na Kieran McKenna ni miongoni mwa makocha waliokuwa kwenye rada ya Man United.

Man United ilimaliza nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu England, ambapo kilikuwa kipindi kibaya zaidi kumaliza ligi tangu mwaka 1990 na ilimaliza mkiani pia kwenye kundi la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu wa 2023-24.

Baada ya kufika fainali ya Kombe la FA na kushinda mbele ya Man City kwa mabao 2-1, hilo  liliokoa kibarua cha Ten Hag kwa muda.

Lakini, mambo yaliendelea kuwa mabaya huko Man United na miezi mitano baadaye, Ten Hag alifutwa kazi na kibarua chake kukabiliwa Ruben Amorim.

Thomas Frank kwa sasa ni kocha wa Tottenham Hotspur.