Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Van de Ven afunga bao la ajabu Spurs ikipiga mtu nne

Muktasari:

  • Mabao kutoka kwa Brennan Johnson na Wilson Odobert yaliwaweka Spurs kifua mbele kwa mabao mawili na kuonekana kama tayari wameimaliza mechi, kabla Johnson kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kuteleza na kumgusa Marcos Lopez kwenye kifundo cha mguu katika mechi hiyo iliyochezwa usiku wa Novemba 4, 2025 kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur.

LONDON, ENGLAND: Tottenham wakiwa na wachezaji 10, wametoa burudani kwenye Ligi ya Mabingwa, sambamba na kufunga bao la kushangaza kutoka kwa beki wa kati Micky van de Ven, walipowacharaza Copenhagen na kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi kwenye mashindano hayo.

Mabao kutoka kwa Brennan Johnson na Wilson Odobert yaliwaweka Spurs kifua mbele kwa mabao mawili na kuonekana kama tayari wameimaliza mechi, kabla Johnson kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kuteleza na kumgusa Marcos Lopez kwenye kifundo cha mguu katika mechi hiyo iliyochezwa usiku wa Novemba 4, 2025 kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur.

Lakini licha ya kucheza wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja, Van de Ven alifunga moja ya mabao bora kabisa ya msimu. Alichukua mpira ndani ya nusu yao ya uwanja na kukimbia hadi mbele, akiwapita wachezaji wanne wa Copenhagen kabla ya kumalizia kwa ustadi ambao hata angekuwa mshambuliaji angejisifia kwa umaliziaji huo.

Spurs walikuwa wamezomewa na mashabiki wao mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Chelsea, lakini safari hii mashabiki walikuwa wamesimama wakishangilia kipindi chote cha pili huku Joao Palhinha akiongeza bao la nne akiwa hajabanwa baada ya kazi nzuri ya Cristian Romero.

Mambo yalikaribia kuwa mazuri zaidi kwa Tottenham walipopewa penalti muda wa majeruhi, lakini Richarlison alikosa nafasi hiyo baada ya kupiga mpira ukagonga mwamba wa juu.

Kwa Van de Ven, ilikuwa ni jibu bora zaidi baada ya kamera za televisheni kumwonyesha akionekana kumpuuza kocha Thomas Frank wakati alipowaomba yeye na Djed Spence kuwasalimia mashabiki wa Spurs baada ya mechi dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita.

Hata hivyo, baada ya wote kuomba msamaha Jumatatu, Van de Ven aliingizwa kwenye kikosi cha kwanza na akafanya tofauti kubwa kwenye mchezo huu.

Ushindi huo unaifanya Tottenham kufikisha pointi nane baada ya mechi nne za Ligi ya Mabingwa, wakiwa na ushindi mara mbili na sare mbili. Mechi inayofuata ni dhidi ya mabingwa watetezi, Paris Saint-Germain, Novemba 26, 2025.

Tottenham wako nafasi ya saba katika msimamo wa UEFA ikiwa ni sehemu nzuri ya kumaliza ndani ya nane bora, jambo litakalowaruhusu kuruka hatua ya mchujo na moja kwa moja kuingia hatua ya 16 bora.