Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha mpya Morocco atuma salamu kwa wachezaji

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF), Fouzi Lekjaa, amesema uamuzi wa kumteua Ouahbi umekuja baada ya tathmini ya kina.

KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Morocco, Mohamed Ouahbi, ameahidi kuendeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana hivi karibuni huku akisisitiza kuwa uteuzi wa wachezaji utazingatia kiwango cha uwanjani na sio umri.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utambulisho wake katika Kituo cha Soka cha Mohammed VI huko Maâmoura, Ouahbi amesema, kipaumbele chake ni kulinda maendeleo yaliyofikiwa na kuiandaa timu hiyo kwa mashindano ya kimataifa yajayo.

“Ninasukumwa na dhamira thabiti ya kuendeleza kazi iliyoanzishwa ili kutumia mafanikio yaliyopatikana kuifanya timu ya taifa ya Morocco izidi kung’ara,” amesisitiza Ouahbi mbele ya waandishi wa habari.

Ouahbi amebainisha kuwa Morocco tayari ina msingi imara unaoweza kushindana na mataifa yenye nguvu zaidi duniani, jambo ambalo litaisaidia nchi hiyo kubaki na ushindani katika michuano mikubwa, ikiwemo Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Katika kuelekea maandalizi ya mechi zijazo, kocha huyo amefafanua kuwa hatachagua mchezaji kwa kuangalia umri wake au ligi anayocheza, bali uwezo na kiwango anachoonyesha uwanjani ndicho kitakuwa kigezo kikuu. Amesema lengo lake ni kuunda kikosi imara na chenye uwiano kitakachoweza kuleta ushindani wa kweli.

Aidha, Ouahbi ameeleza kuwa anahisi ana deni kubwa la kimaadili kwa nchi ya Morocco kuliko hata mkataba wa kimaandishi. Katika hafla hiyo, alimtambulisha João Sacramento kama msaidizi wake wa kwanza, huku akiahidi kutangaza benchi zima la ufundi hivi karibuni.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF), Fouzi Lekjaa, amesema uamuzi wa kumteua Ouahbi umekuja baada ya tathmini ya kina.

“Tumetoa kipaumbele kwa mwendelezo,” amesema Lekjaa, akiongeza kuwa imani ya shirikisho kwa wataalamu wa ndani imeanza kuzaa matunda chanya katika soka la Morocco.