Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Misri amtumainia Salah, alipotezea sakata la Liverpool

HOSSAM Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa Misri yupo katika michuano hiyo inayoanza usiku huu huko Morocco baada ya tukio la msuguano mkubwa kufuatia kuachwa kwake na mabingwa wa Ligi Kuu ya England, lakini kauli zake pamoja na kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake hazijaathiri kiwango chake, Hassan amesema kabla ya mechi ya kwanza ya Kundi B dhidi ya Zimbabwe, itakayochezwa kesho huko Agadir.

KOCHA Mkuu wa Misri, Hossam Hassan amesema anaamini nahodha wa timu hiyo, Mohamed Salah, ameweka kando changamoto za hivi karibuni alizokuwa nazo Liverpool na sasa anaelekeza nguvu katika kusaka mafanikio kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 akiwa na timu hiyo ya taifa itakayofungua dimba kwa kuumana na Zimbabwe kesho Jumatatu usiku.

Nyota huyo wa Misri yupo katika michuano hiyo inayoanza usiku huu huko Morocco baada ya tukio la msuguano mkubwa kufuatia kuachwa kwake na mabingwa wa Ligi Kuu ya England, lakini kauli zake pamoja na kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake hazijaathiri kiwango chake, Hassan amesema kabla ya mechi ya kwanza ya Kundi B dhidi ya Zimbabwe, itakayochezwa kesho huko Agadir.

"Morali ya Salah katika mazoezi iko juu sana, kana kwamba ndio kwanza ameanza kuchezea timu hii ya taifa na naamini atafanya makubwa akiwa na nchi yake,” amesema kocha huyo.

Akiwa na umri wa miaka 33, hii huenda ikawa nafasi ya mwisho kwa Salah kutwaa taji ambalo limekuwa likimponyoka na Misri na kuongeza mafanikio ya kimataifa katika msako wake mkubwa wa medali za ngazi ya klabu.

“Ninaamini Salah atakuwa miongoni mwa wachezaji bora katika mashindano haya na ataendelea kuwa nembo na mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani," amesema Hassan na kuongeza;

“Ninamuunga mkono kitekniki na kisaikolojia, kwa sababu hatuwezi kusahau kuwa Salah anahitaji kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika.”

HOSSA 01

Salah anaingia katika mechi ya Jumatatu baada ya mara ya mwisho kuanza kikosi cha Liverpool katika kipigo cha 4-1 nyumbani dhidi ya PSV Eindhoven , mechi ya Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa Novemba.

Aliachwa katika mechi iliyofuata dhidi ya West Ham United na baada ya sare dhidi ya Leeds United Desemba 6, aliishambulia vikali klabu hiyo pamoja na kocha Arne Slot, akiwaambia waandishi wa habari, alihisi amefanywa kuwa kafara kwa mwanzo mbaya wa msimu na kudokeza kuwa huenda muda wake Anfield haukuwa mrefu tena.

Hassan amesema alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na nahodha wake wakati wa sakata hilo.

“Kulikuwa na mawasiliano ya kudumu na Mohamed Salah katika kipindi ambacho sitaki kukiita mgogoro, kwa sababu mchezaji yeyote anaweza kuwa na tofauti ya maoni na kocha wake akiwa klabuni,” amesema Hassan.

HOSSA 02

Salah hajafunga bao tangu ushindi wa Liverpool 2-0 dhidi ya Aston Villa mwanzoni mwa Novemba, ikiwa ni pamoja na mechi ya kirafiki aliyocheza na Misri dhidi ya Uzbekistan mwezi uliopita.

"Hali kama hiyo hiyo iliwahi kumpata Salah alipokuwa akipitia kipindi cha kukosa mabao akiwa Liverpool," Hassan aliwaambia waandishi wa habari na kuongeza;

“Kisha alirudi kwenye mstari sahihi kupitia timu ya taifa, na matokeo yake akarudi akiwa kwenye kiwango bora zaidi kuliko hapo awali. Ninaamini atafanya mashindano makubwa pamoja na wachezaji wenzake.”

Salah akiwa na Misri amewahi kumliza kama washindi wa pili wa AFCON mara mbili, mwaka 2017 na 2021.

Misri imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mara saba, idadi kubwa kuliko taifa lolote, lakini mafanikio yao ya mwisho yalikuwa mwaka 2010.