Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Manchester City hataki Haaland apumzike

PEP Pict

Muktasari:

  • Msimu wa kutumika bila ya kupumzika kwa Haaland ulianza Juni  katika Kombe la Dunia la Klabu na huenda ukamalizika Marekani majira ya kiangazi mwakani ikiwa taifa lake, Norway litafukuzu kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri anaumia sana kuona straika wake Erling Haaland akicheza mechi nyingi mfululizo, lakini hawezi kumpumzisha kwa sasa.

Tangu kuanza kwa msimu huu, hakuna mchezaji aliyeanza mechi nyingi zaidi au kucheza dakika nyingi zaidi katika kikosi cha Manchester City kumzidi Haaland, ambaye pia amecheza karibu dakika zote katika mechi nne za kufuzu Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Norway tangu Juni mwaka huu. Licha ya kutumika kiasi hicho, Man City haitaki kabisa kumpumzisha fundi huyu kutokana na umuhimu wake kikosi cha kwanza.

Mechi pekee ambayo Haaland hakuanza kikosi cha Man City tangu Juni   ni ile ya Carabao Cup dhidi ya Huddersfield.

PE 01

Msimu wa kutumika bila ya kupumzika kwa Haaland ulianza Juni  katika Kombe la Dunia la Klabu na huenda ukamalizika Marekani majira ya kiangazi mwakani ikiwa taifa lake, Norway litafukuzu kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28.

Kijumla, staa huyu anatarajiwa kucheza zaidi ya mechi 70 msimu huu ikiwa atacheza na Kombe la Dunia, jambo lililosababisha kocha wa timu ya taifa ya Norway kusema angependa kuona anapumzishwa kidogo, lakini Guardiola amesisitiza hawezi kufanya hivyo kwa sasa, labda hapo baadae ikiwa timu yake itakuwa imejihakikishia ubingwa wa ligi mapema.

PE 02

"Ninaumia sana ninapoona anacheza sana, lakini kwa sasa sifikirii suala hilo la kumpumzisha. Labda mwishoni, naweza kufanya hivyo ikiwa tutajihakikishia kushinda Ligi Kuu England kabla ya msimu kumalizika," amesema Guardiola.

PE 03

"Vilevile ukiangalia kwa sasa Haaland anajisikia vizuri, yuko fiti. Zipo mechi ambazo tutaona amechoka na hatutomchezesha. Lazima watu wafahamu tupo katika hatua muhimu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na  mechi mbili zijazo za nyumbani zitaamua ikiwa tutamaliza ndani ya timu nane bora au laa."