Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Manchester City amkingia kifua Donnarumma

PEP Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo wa kimataifa wa Hispania alimsifu kipa huyo wa Italia kwa utulivu wake, udhibiti na uchezaji wa pasi fupi, akisema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ni "bora sana kuliko watu wanavyodhan.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amemlinda kipa wake Gianluigi Donnarumma ambaye amekuwa akikosolewa kwa pasi zake fupi anazopiga kwenda kwa mabeki.

Kocha huyo wa kimataifa wa Hispania alimsifu kipa huyo wa Italia kwa utulivu wake, udhibiti na uchezaji wa pasi fupi, akisema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ni "bora sana kuliko watu wanavyodhan.

Hata hivyo, Guardiola alikiri kuwa urefu wa pasi za Donnarumma hauwezi kulinganishwa na ule wa kipa wa zamani wa timu hiyo, Mbrazil Ederson ambaye kwa sasa anaitumikia Fenerbahce.

Ingawa uwezo wa Donnarumma kuokoa mipira ni mkubwa, wachambuzi wengi wamekuwa wakimkosoa kwa namna anavyocheza akiwa na mpira mguuni.

PE 01

Donnarumma alijiunga na Man City kwa  uhamisho wa Pauni 26 milioni mwaka jana baada ya kutokea kwa kile kilichoelezwa kuwa aligombana na kocha wa PSG, Luis Enrique ambaye hakua anamhitaji katika kikosi chake licha ya kipa huyo kuisaidi timu kushinda taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa.

Baada ya kuondoka kwa Donnarumma PSG iliamua kumpa nafasi kipa wao namba mbili Lucas Chevalier ambaye ndio tegemeo kwa sasa.

Man City walitengeneza nafasi ya kumsajili Donnarumma kwa kumuuza Ederson kwenda Fenerbahce kwa Pauni 10 milioni 10.

Kutokana na historia ya Guardiola ya kupendelea makipa  wenye sifa za kupiga pasi, uamuzi wake wa kumsaijili Donnarumma uliibua mashaka

PE 02

Hata hivyo, katika mkutano wa waandishi wa habari kabla ya mechi ya FA Cup dhidi ya Exeter City, Guardiola amesema:"Donnarumma ni kipa mzuri sana na mwenye kupiga pasi fupi na zenye kasi. Hawezi kupiga pasi ndefu kama Ederson, lakini hakuna kipa mwingine anayepiga pasi kama Ederson. Lakini Donnarumma ni mzuri sana katika kupooza mashambulizi, ana uwezo mzuri wa kumiliki mpira na kufanya maamuzi ya haraka ya kupiga pasi fupi kwenye sekta hizo ni bora zaidi kuliko watu wanavyodhani."

Hata hivyo, takwimu zinaonyesha  Ederson ana wastani mzuri zaidi kuliko Donnarumma. Alikuwa na  wastani wa kupiga pasi kwa asilimia 31.7 dhidi ya 23.4 zile za Donnaruma kwa kila dakika 90 katika msimu wa 2024/25.

 Mbrazil huyo pia alipiga pasi ndefu nyingi zaidi 9.4 dhidi ya 6 sita za Donnarumma  na kwa usahihi zaidi za asilimia 57.92% dhidi ya 44.6% zile za Donnarumma alizokuwa nazo katika msimu wake wa mwisho. akiwa na PSG.