Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Chelsea afichua jambo zito

MARESCA Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Italia mwenye umri wa miaka 45 alikataa kusema wazi ni nani aliyekuwa hampi sapoti, lakini baadhi ya ripoti zinadai kuna uwezekano mkubwa ikawa ni wamiliki wa klabu hiyo.

LONDON, ENGLAND:KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amesema siku mbili zilizopita zilikuwa ‘mbaya zaidi’ katika kipindi chake cha ukocha wa klabu hiyo, akidai kuwa alikosa sapoti kutoka kwa baadhi ya watu wa timu hiyo.

Kocha huyo raia wa Italia mwenye umri wa miaka 45 alikataa kusema wazi ni nani aliyekuwa hampi sapoti, lakini baadhi ya ripoti zinadai kuna uwezekano mkubwa ikawa ni wamiliki wa klabu hiyo.

Chelsea ilikuwa haijashinda mechi nne mfululizo kabla ya Cole Palmer kufunga bao lake la kwanza tangu Septemba, lililoiwezesha kushinda mechi dhidi ya Everton wikiendi iliyopita kwa mabao 2-0.

“Kuanzia nilipojiunga na klabu hiyo, saa 48 zilizopita ndio zilikuwa mbaya zaidi tangu wakati huo, kwa sababu watu wengi hawakuwa wakituunga mkono tena, hawakuwa wakinitia moyo mimi na wachezaji wangu.”

Kocha huyu alipoulizwa kama alikuwa akikosa sapoti kutoka ndani ya klabu, amesema “Ni kwa ujumla. Kwa ujumla. Nawapenda mashabiki na tunafurahia sana sapoti yao.”

Chelsea sasa imecheza mechi tano ndani ya siku 12, huku ushindi wao wa jana ukiwa ndio pekee katika kipindi hicho.

Kipigo dhidi ya Leeds inayopambana kuepuka kushuka daraja kilionekana kukera mashabiki wengi na Maresca amesema yeye ndio anapaswa kuwajibika kwa matokeo hayo.

“Ninajaribu kuwashawishi wachezaji kwamba huu ni mpira wa miguu. Kinachoendelea ni sehemu ya mpira wa miguu. Unahitaji kuwa tayari. Niliwajibika kwa 100% kwa matokeo.”

“Kwa mechi dhidi ya Leeds ilikuwa ni kosa langu, kuanzia mpango wa mchezo na maandalizi ya mechi kwa ujumla. Halikuwa kosa la wachezaji. Tunaendelea kuongezeka ubora zaidi na zaidi, hasa katika wakati huu ambao tumekuwa tukipata matokeo mabaya.”