Mastaa NBA walivyobadili timu usajili ukifungwa
Muktasari:
- Tofauti na usajili katika soka, NBA kinachofanyika ni ubadilishanaji wa wachezaji kibiashara au utoaji wa mchezaji ama wachezaji kwa timu nyingine kisha malipo au makubaliano ya kibiashara hufanyika.
CHICAGO, MAREKANI: DIRISHA la mwisho la usajili wa wachezaji la 2026 lilifungwa wiki iliyopita, huku timu 27 kati ya 30 za ligi hiyo zikifanya biashara (trades) katika wiki ya mwisho. Hizi hapa baadhi ya takwimu muhimu kuhusu timu zilizofanya mabadiliko na wachezaji waliobadilishwa.
Tofauti na usajili katika soka, NBA kinachofanyika ni ubadilishanaji wa wachezaji kibiashara au utoaji wa mchezaji ama wachezaji kwa timu nyingine kisha malipo au makubaliano ya kibiashara hufanyika.
KANDA YA MAGHARIBI
ATLANTA HAWKS
WAMEINGIA: Buddy Hield, Jonathan Kuminga, Jock Landale, Gabe Vincent
WAMETOKA: Luke Kennard, Vít Krejci, Kristaps Porzingis
Muhtasari: Hawks wanajenga upya kikosi baada ya biashara ya Trae Young mwezi uliopita, na wameamua kumjaribu Kuminga mwenye mwili mkubwa ambaye hakuwahi kupata nafasi kubwa wakati akiwa Golden State Warriors.
Takwimu: Kuminga ana asilimia 49.5 ya ufikiaji goli katika misimu miwili iliyopita akiwa ameshuka kutoka 56.7 katika misimu mitatu iliyotangulia. Hata hivyo, kiwango chake cha mitupo ya mbali kinamuweka nafasi ya 15 kati ya wachezaji 135 wenye urefu wa futi 6–8 au chini waliorusha mipira mara 2,000 katika miaka mitano iliyopita.
kwa upande wake ana asilimia 23.1 ya ribaundi za kushambulia katika dakika za mwisho za mechi zenye tofauti ya pointi tano au chini kikiwa ni kiwango cha juu zaidi kati ya wachezaji 193 waliocheza angalau mechi 12 za “clutch”.
BOSTON CELTICS
WAMEINGIA: Nikola Vucevic
WAMETOKA: Anfernee Simons, Xavier Tillman
Muhtasari: Licha ya kumkosa Jayson Tatum na kuachana na wachezaji kadhaa, Celtics wana tofauti bora ya pointi Kanda ya Mashariki. Kubadilishana Simons kwa Vucevic kunajaza nafasi muhimu Celtics na kunapaswa kuwabakisha katika tatu bora kwa ufanisi wa ushambuliaji.
Takwimu: Celtics wako mwisho mwa ligi katika namba nyingi uwanjani. Vucevic alikotoka hakuwa na mchango mkubwa. Hata hivyo, ni mkali wa ribaundi akishika nafasi ya 18 kati ya wachezaji 219 waliocheza angalau dakika 20 kwa mchezo.
CHARLOTTE HORNETS
WAMEINGIA: Malaki Branham, Xavier Tillman, Coby White
WAMETOKA: Mason Plumlee, Collin Sexton
Muhtasari: Hornets wameongeza ushindi hadi michezo minane mfululizo, na wamekuwa na ushindi wa 20–7 wakati LaMelo Ball, Brandon Miller na Kon Knueppel wanapoanza pamoja. Kubadilisha Sexton kwa White kumeimarisha benchi lao, na sasa wako kwenye nafasi ya 'play-in'.
Takwimu: Hornets ndio timu iliyoboreshwa zaidi ligi nzima ikiwa bora kwa pointi 11.0 kwa kila mashambulizi 100 ukilinganisha na msimu uliopita.
CLEVELAND CAVALIERS
WAMEINGIA: Keon Ellis, James Harden, Emanuel Miller, Dennis Schröder
WAMETOKA: Lonzo Ball, Darius Garland, De’Andre Hunter
Muhtasari: Cavs wamekuwa miongoni mwa timu zilizokatisha tamaa wengi msimu huu, lakini wameshinda mechi 14 kati ya 19 za hivi karibuni. Kumbadilisha Garland dhidi ya Harden ni hatua bora, ambapo Harden, licha ya kuwa mkubwa kwa miaka 10, amekuwa na uimara zaidi.
Takwimu: Kumekuwapo na kuporomoka kwa alama kwa Cavs zaidi wakati Donovan Mitchell asipokuwa uwanjani.
Lakini, Ellis ana asilimia 41.6 ya mitupo ya 3-point katika miaka minne iliyopita akishika nafasi ya sita kati ya wachezaji 236. Harden amefanya jambo ambalo hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufanya zaidi ya mara moja katika historia ya mstari wa pointi tatu. Cavs wako juu kwa mikimbio wakiwa na mpira na wachezaji, tofauti na timu nyingi alizocheza Harden.
DETROIT PISTONS
WAMEINGIA: Kevin Huerter
WAMETOKA: Jaden Ivey
Muhtasari: Ivey amekuwa bora zaidi mitupo ya 3-point kuliko Huerter misimu miwili iliyopita, lakini Huerter anaongeza ubora na uwezo wa mitupo akisogea jirani ya nyavu.
Takwimu: Pistons wako nafasi ya 28 kwa 3-point. Huerter anana asilimia 55.2 ya mitupo ya 3-point, lakini kwa asilimia 31.4, kiwango cha chini kabisa tangu aanze kucheza kikapu.
INDIANA PACERS
WAMEINGIA: Kobe Brown, Ivica Zubac
WAMETOKA: Isaiah Jackson, Bennedict Mathurin
Muhtasari: Pacers hatimaye wamepata mbadala wa Myles Turner. Zubac ana nguvu kwenye 'pick-and-roll' na ataleta uthabiti eneo la ulinzi.
Takwimu: Zubac ana asilimia 18.0 ya ribaundi zote akiwa uwanjani (akishika nafasi ya 8 NBA). Ana asilimia 97.7 ya mitupo bora ndani ya eneo la mpinzani kikiwa ni kiwango cha juu zaidi katika ligi hiyo.
WASHINGTON WIZARDS
WAMEINGIA: Anthony Davis, Dante Exum, Jaden Hardy, D’Angelo Russell
WAMETOKA: Marvin Bagley III, Malaki Branham, AJ Johnson, Khris Middleton
Muhtasari: Baada ya kumpata Trae Young, Wizards wamemuongeza Anthony Davis wakijenga mchanganyiko wa uzoefu na vipaji chipukizi. Umathubuti kiafya itakuwa swali kubwa.
Takwimu: Davis ni mmoja wa wachezaji wawili tu katika historia ya NBA (pamoja na Kareem Abdul-Jabbar) waliocheza mechi 500+ na wastani wa pointi 24, ribaundi 10 na 'bloki' 2 katika taaluma yao. Ana asilimia 61.9 ya mitupo ndani ya eneo la mpinzani lakini ni 40.5 akiwa nje.
Western Conference
LOS ANGELES CLIPPERS
WAMEINGIA: Darius Garland, Isaiah Jackson, Bennedict Mathurin
WAMETOKA: Kobe Brown, James Harden, Chris Paul, Ivica Zubac
Muhtasari: Clippers wameamua kubadili mwelekeo licha ya kuwa na rekodi bora kipindi cha hivi karibuni. Garland ni mdogo kwa miaka na ana mkataba mrefu zaidi.
Takwimu: Garland ni mmoja wa wachezaji wanne pekee wenye wastani wa pointi 17 na asisti 6 katika misimu sita mfululizo.
LOS ANGELES LAKERS
WAMEINGIA: Luke Kennard
WAMETOKA: Gabe Vincent
Muhtasari: Lakers wamemchukua Luka Doncic mrushaji mzuri zaidi wa mitupo ya nje.
Takwimu: Nyota mpya, Kennard ana asilimia 46.0 ya 3-point katika misimu mitano iliyopita na bora kuliko wachezaji 274. Ana asilimia 51.2 ya upokonyaji mipira msimu huu kikiwa ni kiwango bora zaidi katika ligi.
MINNESOTA TIMBERWOLVES
WAMEINGIA: Ayo Dosunmu, Julian Phillips
WAMETOKA: Mike Conley, Rob Dillingham, Leonard Miller
Muhtasari: Dosunmu anaongeza uzoefu na mchango wa pande zote mbili za uwanja maeneo anayopenda kushambulia.
Takwimu: Dosunmu ambaye ni usajili mpya ana rekodi bora kwa pointi kwa dakika 36 (pointi 20.5) na pasi bora awapo eneo lolote la uwanja (asilimia 63.6). Pia ana asilimia 45.1 ya 3-point akiwa nafasi ya sita katika ligi.
OKLAHOMA CITY THUNDER
WAMEINGIA: Jared McCain, Mason Plumlee
WAMETOKA: Ousmane Dieng
Muhtasari: Thunder wametumia chaguo lao la drafti kumpata McCain.
Takwimu: McCain ndiye mchezaji pekee wa mwaka wa pili mwenye asilimia 40+ ya kudaka na kurusha mpira wakati huohuo katika misimu miwili mfululizo.
PORTLAND TRAIL BLAZERS
WAMEINGIA: Vit Krejci
WAMETOLEA: Duop Reath
Muhtasari: Blazers wameimarisha kikosi chao upande wa ulinzi kwa kumpata mtu mahiri.
Takwimu: Krejci ana asilimia 42.4 mitupo ya 3-point katika misimu mitatu iliyopita akiwa ndani ya nafasi ya nne bora.
UTAH JAZZ
WAMEINGIA: Jaren Jackson Jr., John Konchar, Vince Williams Jr.
WAMETOKA: Kyle Anderson, Walter Clayton Jr., Taylor Hendricks, Georges Niang
Muhtasari: Jazz wamejilipua ili kuboresha ushindani kwa kumnasa Jackson.
Takwimu: Jackson ndiye mchezaji pekee aliyecheza mechi 250+ katika misimu mitano iliyopita na wastani wa pointi 18 na 'block' 2.