Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Klopp hajafunga mlango wa kutua Real Madrid

KLOP

Muktasari:

  • Klopp aliacha kazi ya ukocha Liverpool 2024, lakini bado anaendelea kuhusishwa na nafasi kubwa za kazi katika soka la kimataifa.

MADRID, HISPANIA: KOCHA Jurgen Klopp amekiri kuwa hawezi kuondoa uwezekano wa kurejea katika ukocha baada ya kuhusishwa na klabu ya Real Madrid.

Klopp aliacha kazi ya ukocha Liverpool 2024, lakini bado anaendelea kuhusishwa na nafasi kubwa za kazi katika soka la kimataifa.

Kwa sasa, Mjerumani huyo anafanya kazi kama Mkuu wa Kimataifa wa Masuala ya Soka wa Red Bull, akisimamia mfumo wao wa klabu nyingi ikiwamo RB Leipzig, New York Red Bulls na Paris FC.

Baada ya kujiondoa kwenye mwanga wa umaarufu, Klopp amekuwa akisisitiza mara kwa mara jinsi alivyoridhika kufanya kazi nyuma ya pazia na Red Bull.

Hata hivyo, sasa ameibuka kama mmoja wa wagombea wanaotajwa kuchukua nafasi Real Madrid kufuatia kufutwa kazi kwa Xabi Alonso wiki iliyopita.

KLO 01

Mabingwa hao wa Hispania walimteua aliyekuwa mchezaji mwenza na rafiki yake wa karibu Alonso, Alvaro Arbeloa, kuwa kocha wao lakini hilo halijazuia tetesi kuendelea.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 alikiri kuwa alipokuwa anaondoka Liverpool, Mei 2024, alikuwa amepoteza nguvu na hamu ya kuendelea na kazi yenye shinikizo kubwa. Hata hivyo, amekataa kufunga kabisa mlango wa kurejea kwenye benchi la ufundi siku zijazo.

“Kwa sasa niko mahali, kama binadamu, ambapo nimeridhika kabisa na nilipo. Sitamani kuwa mahali pengine,” Klopp aliiambia AFP.

“Siamki kwa msisimko nikisikia Real Madrid wanaonyesha nia. Hata kama wangekuwa wanaonyesha, hilo ni suala la vyombo vya habari.

“Je, nataka kufundisha tena? Kwa sasa ningesema hapana, lakini siwezi kusema kamwe, kamwe, kamwe. Sitarajii kubadilisha mawazo yangu, lakini sijui.”

Kwa mujibu wa Sky Sports, Klopp anazingatiwa na Real Madrid, ambao huenda wakajaribu kumshawishi. Kocha huyo wa zamani wa Liverpool pia alitoa tathmini yake ya jumla kuhusu hali ilivyo katika mji mkuu wa Hispania.

KLO 02

“Niliposikia habari za Xabi Alonso, nilihisi mchanganyiko wa hisia,” amesema Klopp.

“Ndiyo, nilishangaa. Na hapana, sikushangaa. Nilijiuliza ‘nini?’ na pia nikasema ‘ndiyo, bila shaka’. Sina uhakika kwa nini ilitokea, lakini kila tukio lina mazingira yake maalum, si tatizo la jumla. Kile wanachokiona sasa Real Madrid ni kwamba kumleta tu mtu mwingine si jambo rahisi.

“Ningependekeza kuwa kama unamfuta kocha, ni bora uwe tayari una wazo la nani atamrithi. Na wazo hilo liwe la kweli. Kama wanafikiria wanaweza kumpata Pep Guardiola, ningesema nafasi ni ndogo sana.”