Klopp amzuia Firmino kuondoka

LIVERPOOL, ENGLAND. KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp anataka fowadi wake Roberto Firmino abaki na hana mpango wa kumuuza siku za usoni kama taarifa zilivyokuwa zikiripoti,

Klopp amesisitiza kuhusu Firmino wapo kwenye mchakato wa kumwongezea mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Anfield.

Nyota huyo wa kimataifa Brazil amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Klopp na amepata mafanikio chini ya kocha huyo, anayeamini Firmino ni zawadi aliyoachiwa na Brendan

Rodgers wakati anatua Anfield mwaka 2015.

Licha ya kumzuia Firmino asiondoke Anfield, Klopp amesisitiza wapo baadhi wa wachezaji watakaoondoka mwisho mwa msimu kama Alex Oxlade-Chamberlain ambaye hataongeza mkataba, isipokuwa Naby Keita kuna uwezekano akabaki.

"Milango ipo wazi kwa kila mtu, mchezaji yoyote mpambanaji ana nafasi ya kucheza, haya si mashindano ya maonyesho, kila mechi ni ushindani, kila mchezaji anajituma, Firmino ni mchezaji mzuri, alipitia kipindi kigumu kawaida kwa mchezaji, Thiago Alcantara na Naby wote wana muhimu pia, wachezaji hawa wana msaada kwenye timu hili ndio jambo kwasasa," alisema Klopp.

Tetesi ziliripoti Firmino ataondoka mwisho mwa msimu kutokana na nafasi chache anazopata chini ya kocha Klopp, lakini sasa kocha huyo hana mpango wa kumuachia mwishoni mwa msimu.

Firmino alikuwa sehemu ya kikosi kilichobeba ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya mwaka 2019, pamoja na Ligi Kuu England.

Baada ya kutawala ndani ya misimu kadhaa iliyopita Liverpool imeanza msimu wa 2022-2023 kwa kusuasua, vijana wa Klopp walipokea kichapo mfululizo dhidi ya Brentford na Brighton, baada ya vipigo hivyo majogoo wa jiji wamejikita nafasi ya tisa wakiwa na pointi 28 kwenye msimamo wa ligi.

Wakati huo huo Liverpool imetinga raundi ya nne ya michuano ya Kombe la FA baada y kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wolves kwenye mchezo wao wa marudiano. Mchezo wao wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.