Klopp aanza kufungasha virago kwa kombe

IKIWA imebakia miezi michache kabla ya kuondoka kwenye kikosi cha Liverpool kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp amepata zawadi ya kuwaachia mashabiki wa timu hiyo.
Klopp amefanikisha hilo baada ya kuwawezesha Majogoo hao kupata ubingwa wa kombe la Carabao kwa kuichapa Chelsea bao 1-0, kwenye mchezo uliopigwa leo katika dimba la Wembley.
Mchezo huo ambao ulimalizika kwa suluhu kwenye dakika 90, uliamuliwa kwenye dakika 30 za nyongeza kwa bao la beki wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk aliyefunga dakika ya 118 kwa kichwa akiunganisha kona ya Konstantinos Tsimikas.
Hilikuwa linakuwa ni taji la tisa kwa Klopp tangu ajiunge na wababe hawa mwaka 2016, ikiwa pia ni lapili kwenye michuano hii ya Carabao baada ya kutwaa la kwanza mwaka 2022.
Kipigo hiki pia kimemuweka kocha wa Chelsea Maurico Pochettino kwenye hatari ya kupoteza kazi kutokana na matokeo mabaya ambayo timu hiyo imekuwa nayo tangu kuanza kwa msimu.