Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Sterling, Chelsea yapigiwa simu kali

SIMU Pict

Muktasari:

  • Sterling na Disasi walijaribu kutafuta suluhu za kuondoka siku ya mwisho wa dirisha la usajili, lakini wakaishia kubaki kwenye kundi linalojulikana kama “Bomb Squad” la klabu hiyo wakiwa hawajaingizwa katika kikosi ambacho kitaichezea Chelsea katika michuano yoyote.

LONDON, ENGLAND: CHAMA cha Wachezaji wa Soka wa Kulipwa (PFA) kinaripotiwa kuwa katika mazungumzo na Chelsea kuhusu jinsi wanavyowatendea wachezaji waliotengwa Raheem Sterling na Axel Disasi.

Sterling na Disasi walijaribu kutafuta suluhu za kuondoka siku ya mwisho wa dirisha la usajili, lakini wakaishia kubaki kwenye kundi linalojulikana kama “Bomb Squad” la klabu hiyo wakiwa hawajaingizwa katika kikosi ambacho kitaichezea Chelsea katika michuano yoyote.

Kwa mujibu wa BBC Sport, PFA wamewasiliana na Chelsea wakitaka kuhakikisha Sterling na Disasi wanapata “mazingira bora ya kufanya mazoezi katika kiwango cha juu” licha ya kutokuwepo katika kikosi cha kwanza.

Chama hicho kinahakikisha kuwa klabu zinafuata masharti makali ya FIFA kuhusu wachezaji wanaotengwa na vikosi vya kwanza ili kuepuka mazingira ya unyanyasaji.

Mkataba wa Sterling, unaomuingizia Pauni 325,000 kwa wiki, unamalizika mwaka 2027, huku ule wa Disasi ukiisha mwaka 2029.

Sterling alikuwa karibu kujiunga na Fulham kwa mkopo, na Disasi alikataa uhamisho kwenda West Ham mapema mwezi huu.

Wote wawili wanaonekana kutokuwa na mustakabali Chelsea, kwani huenda wasichezee kikosi cha kwanza kwa miezi kadhaa ijayo.

Taarifa zinaongeza kuwa Chelsea, ambayo inafanya kazi kwa karibu na PFA, iliwasilisha na Sterling na kujadiliana naye uwezekano wa kuhamia Bayern Munich na Napoli katika majira ya kiangazi yaliyopita lakini mchakato ukafeli kwa sababu mbalimbali. Pia, Bayer Leverkusen na Galatasaray zilionyesha nia ya kumtaka.

Disasi alihitajika na West Ham na Bournemouth lakini aliamua kukataa ofa zao.

Inaripotiwa kuwa Sterling na Disasi wamepangiwa nyakati maalum za mazoezi pamoja na kocha mmoja wa Chelsea atakayefanya nao kazi kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.

Wakati huo huo, kikosi cha kwanza cha Chelsea kitasafiri kwenda kumenyana na Manchester United kwenye Ligi Kuu England Jumamosi hii.