Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Rosenior, Scholes aiponda Chelsea

Muktasari:

  • Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Rosenior kufukuzwa kazi kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya, ambapo alipoteza mechi tano mfululizo za Premier League bila hata kufunga bao. Kocha huyo alikaa madarakani kwa takribani miezi mitatu na nusu pekee tangu alipoteuliwa Januari mwaka huu.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes ameishambulia vikali bodi ya Chelsea akidai ilikuwa ‘kichaa’ kumteua Liam Rosenior kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Rosenior kufukuzwa kazi kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya, ambapo alipoteza mechi tano mfululizo za Premier League bila hata kufunga bao. Kocha huyo alikaa madarakani kwa takribani miezi mitatu na nusu pekee tangu alipoteuliwa Januari mwaka huu.

Rosenior alipewa mkataba wa miaka sita na nusu na wamiliki wa Chelsea, BlueCo, wakimchukua kutoka klabu dada ya Strasbourg, lakini mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa.

Katika taarifa ya klabu hiyo baada ya kumtimua, Chelsea ilikiri sasa inaingia katika mchakato wa kujitathmini ili kupata kocha sahihi wa muda mrefu. Pia inaelezwa klabu hiyo imetambua kuwa kumteua kocha asiye na uzoefu mkubwa ilikuwa ni kosa.

Akizungumza kwenye kipindi cha The Overlap Fan Debate, Scholes alisema hakuna mtu mwingine katika dunia ya soka aliyekuwa anaamini Rosenior alikuwa chaguo sahihi kwa Chelsea.

“Siielewi Chelsea wanataka kufanya nini. Kama ni kukuza wachezaji vijana, je hiyo ndiyo njia sahihi? Sijui,” alisema Scholes.

Aliongeza: “Wamiliki watalaumiwa kwa hili. Mbali nao, hakuna aliyefikiri Rosenior alikuwa mtu sahihi kwa Chelsea. Kwangu ilikuwa ajabu sana.”

Kwa sasa, kocha wa muda Calum McFarlane amepewa jukumu la kuinoa timu hiyo na tayari ameipeleka fainali ya Kombe la FA baada ya ushindi dhidi ya Leeds United.

Majina ya makocha kama Xabi Alonso, Andoni Iraola na Marco Silva yanatajwa kuwania nafasi ya ukocha wa kudumu.

Chelsea kwa sasa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi, ikiwa pointi 10 nyuma ya tano na pointi mbili nyuma ya Brighton & Hove Albion. Itarejea uwanjani Mei 4 kuvaana na Nottingham Forest.