Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa mechi ya ufunguzi, Shearer amvaa Alexander Isak

ISAK Pict (1)

Muktasari:

  • Isak amekataa kuichezea Newcastle ikiwa ni katika jaribio la kulazimisha kuondoka, baada ya kuona klabu hiyo imekataa ofa ya awali kutoka Liverpool mwanzoni mwa mwezi huu.

NEWCASTLE, ENGLAND: LEJENDI wa Newcastle United, Alan Shearer amemkosoa straika wa timu hiyo, Alexander Isak baada ya kushindwa kucheza mechi ya ufunguzi wa Newcastle Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa ikiwa ni mwendelezo wa sakata lake la  kuhamia Liverpool.

Isak amekataa kuichezea Newcastle ikiwa ni katika jaribio la kulazimisha kuondoka, baada ya kuona klabu hiyo imekataa ofa ya awali kutoka Liverpool mwanzoni mwa mwezi huu.

Shearer amekosoa tabia ya Isak baada ya kutocheza mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa suluhu na katika mjadala ambao ulianza kwa Wayne Rooney kutoa mtazamao wake akisema Isak amefanya jambo zuri kwani hata yeye alishawahi kufanya hivyo akiwa na Man United, Shearer alijibu:

“Lakini kawaida unawasilisha ombi la kuondoka na siyo kukataa mazoezi au kucheza. Kuna njia za kupita na Alex hajafuata njia sahihi kabisa. Lazima uwe na huruma kwa wachezaji wenzako pamoja na kocha. Wachezaji wanaonekana wanapambana kwa ajili ya timu na maelfu ya mashabiki waliosafiri hadi Villa Park kutazama mechi, lakini upande mwingine wanamwangalia mchezaji mwenzao ambaye amekataa kucheza licha ya kuwa na mkataba wa miaka mitatu na mshahara wa zaidi ya Pauni 100,000 kwa wiki.”

“Mashabiki wanatoa kati ya Pauni 60 hadi 70 kwa tiketi moja ya kuingia uwanjani, pia wanalipa Pauni 30 kwa ajili ya kuweka mafuta katika magari yao au kukata tiketi ya treni. Unaweza kuona jinsi wanavyojisikia pale mchezaji anapoamua tu hachezi. Hilo haliwezi kuwa jambo sahihi kwa mtu ambaye bado ana mkataba wa miaka mitatu.”

“Ninaelewa pia kuna pande mbili za kila hadithi na hatujawahi kusikia lolote kutoka kwake au upande wa wawakilishi wake, yote ni taarifa zilizotolewa kwa njia za siri. Bado kuna uwezekano, ingawa mdogo, anaweza kuunganishwa tena na timu ikiwa ataomba msamaha.”

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe alitoa taarifa kuhusu hatima ya Isak baada ya mchezo, akisema: “Hakuna kilichobadilika. Mlango bado umefunguliwa kabisa lakini lazima aamue anachotaka kufanya. Tunataka suluhisho ambalo ni yeye anayetakiwa kulitoa.”