Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinachokwamisha dili la Wirtz Anfield

WITZ Pict
WITZ Pict

Muktasari:

  • Liverpool na upande wa mchezaji huyo wamekubaliana juu ya mkataba hadi 2030, lakini inaelezwa kwamba changamoto inayosababisha dili hilo lichelewe ni bei yake.

LIVERPOOL, ENGLAND: NYOTA wa kimataifa wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz 22, tayari amefikia makubaliano na mabingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool, lakini changamoto inatajwa kuwa ni ada ya uhamisho.

Liverpool na upande wa mchezaji huyo wamekubaliana juu ya mkataba hadi 2030, lakini inaelezwa kwamba changamoto inayosababisha dili hilo lichelewe ni bei yake.

Hivi karibuni Leverkusen ilikataa ofa ya Liverpool inayodaiwa kufikia Euro 130 milioni ambayo inaamini bado ni ndogo kulingana na ubora alionao.

Inaelezwa licha ya kiasi hicho cha pesa kuonekana kuwa kikubwa, kwa upande wa mabosi wa Leverkusen wanaona bado kabisa hawajakubali kwani wanahitaji dau nono zaidi.

Liverpool inataka kutoa Euro 135 milioni, lakini Bayer bado inasisitiza dau la Euro 150 milioni ambalo ndilo linaihitajika ili kumuuza Wirtz ni kubwa zaidi.

Hata hivyo, hadi sasa bado haijajulikana ikiwa kiasi hicho cha Euro 150 milioni Leverkusen inataka kilipwe kwa awamu ngapi.

Kwa mujibu wa BILD, hakuna mpango wa kufanya mabadilishano ya wachezaji na kiasi cha pesa kwa ajili ya Wirtz baina ya timu hizo kwa sababu mkurugenzi wa michezo wa Leverkusen, Simon Rolfes anachotaka kwa sasa ni pesa na si kingine.

Hadi sasa Wirtz bado hajafanya hata vipimo vya afya licha ya kuwa tayari kujiunga na Majogoo wa Jiji la Liverpool na inaelezwa Leverkusen ipo tayari kuendelea kusalia na mchezaji huyo kwa msimu mmoja zaidi ikiwa haitapata ofa sahihi inayoanzia Euro 150 milioni.