Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikosi bora cha kulipwa hiki hapa

KIKOSI Pict

Muktasari:

  • Zaidi ya wanasoka 20,000 wa kulipwa duniani kote walikuwa na nafasi ya kupiga kura ya kupata mastaa wa kuunda kikosi hicho, ambacho kilizingatia ubora wa wachezaji hao na kile walichofanyika hadi kufikia Agosti 3, 2025.

LONDON, ENGLAND: MASTAA wawili wa England, Jude Bellingham na Cole Palmer wametajwa kwenye Kikosi Bora cha Wanasoka wa Kulipwa Cha Mwaka 2025 (2025 Fifpro World Best XI).

Zaidi ya wanasoka 20,000 wa kulipwa duniani kote walikuwa na nafasi ya kupiga kura ya kupata mastaa wa kuunda kikosi hicho, ambacho kilizingatia ubora wa wachezaji hao na kile walichofanyika hadi kufikia Agosti 3, 2025.

Kwenye orodha hiyo kulikuwa na majina ambayo haikushangaza kuyaona yakihusishwa mshindi wa Ballon d’Or, Ousmane Dembele na aliyeshika namba mbili Lamine Yamal, ambao watacheza kwenye wingi ya kushoto na kulia katika kikosi hicho, huku kukiwa na majina ya mastaa waliotazamiwa wangejumuishwa, lakini wamewekwa kando.

Straika, Harry Kane bado anahesabika kama mmoja wa wachezaji bora kabisa wa England, lakini jina lake limeshindwa kupenya kwenye kikosi hicho cha wachezaji 26.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 32 aliisaidia Bayern Munich kushinda taji la Bundesliga msimu uliopita na amekuwa kwenye kikosi bora pia akiwa na timu ya taifa ya The Three Lions.

Lakini, hayupo kwenye orodha ya washambuliaji nane waliochaguliwa katika kikosi hicho, kundi linalowahusisha pia supastaa wa Inter Miami, Lionel Messi na wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo.

Staa wa Real Madrid, Kylian Mbappe amechaguliwa kuongoza safu ya washambuliaji watatu katika kikosi hicho, huku mchezaji mwenzake wanayecheza pamoja katika chama la Los Blancos, Jude Bellingham ni miongoni mwa wanaounda timu hiyo, wakati Ligi Kuu England imeingiza wakali watatu, akiwamo mkali wa The Blues, Cole Palmer.

Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk ni mmoja ya wanaounda safu ya ulinzi ya mabeki wa tatu, sambamba na mastaa wawili wa Paris Saint-Germain, Nuno Mendes na Achraf Hakimi.

Mchezaji mpya wa Manchester City, kipa Gianluigi Donnarumma, ambaye alishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na PSG msimu uliopita, amechaguliwa kukaa golini.

Kukamilisha kikosi cha kwanza cha timu hiyo, kiungo fundi wa boli wa PSG, Vitinha na mwenzake wa Barcelona, Pedri, wataungana na Palmer na Bellingham kwenye safu ya viungo wanne. Trent Alexander-Arnold alikuwa Mwingereza pekee aliyeingia kwenye kinyang'anyiro, lakini alishindwa kupata nafasi ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza.