Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikao cha Pep, Salah chashtua

Kikao Pict
Kikao Pict

Muktasari:

  • Guardiola alimshuhudia Mo Salah akipeleka kilio kwenye kikosi chake cha Manchester City, wakati alipoisaidia Liverpool kupata ushindi muhimu wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika uwanjani Etihad.

MANCHESTER, ENGLAND: PEP Guardiola amewashtua mashabiki wa Liverpool baada ya picha yake akiwa kwenye kikao cha siri na mshambuliaji wa timu hiyo, Mohames Salah huko Etihad kuonekana hadharani.

Guardiola alimshuhudia Mo Salah akipeleka kilio kwenye kikosi chake cha Manchester City, wakati alipoisaidia Liverpool kupata ushindi muhimu wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika uwanjani Etihad.

Katika mechi hiyo, Mo Salah alifunga na kuasisti na hivyo kuifanya Liverpool kuongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya Arsenal inayoshika nafasi ya pili.

Lakini, kilichowashtua mashabiki ni kumwona Guardiola akiwa na Salah kwenye korido za Etihad baada ya mechi hiyo, huku ikifahamika wazi staa huyo wa Misri amebakiza miezi michache tu kabla ya mkataba wake kufika tamati huko Anfield, ambapo utamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mashabiki baada ya kuona hilo waliwakuwa na maoni tofauti, wakitia mashaka lisitokee wasilopenda litokee.

Shabiki wa kwanza aliandika kwenye mtandao wa X: "Pep Guardiola, usifanye kitu kibaya tafadhali."

Mwingine alisema: "Pep anakitambua kiwango cha dunia cha Mo!"

Na shabiki wa tatu alisema: "Anavunja ukuta wa timu yake kila mwaka, lakini bado Pep anamkubali."

Shabiki wa nne, ambaye dhahiri alionekana kuwa wa Liverpool alisema: "Hebu muache huko."

Mwingine alisema: "Guardiola ni kama anasema, 'hebu njoo tumalize hii kitu pamoja.'"

KIK

Kiwango hicho cha Salah uwanjani Etihad kimemfanya afikishe mabao 30 na asisti 21 katika mechi 38 alizocheza msimu huu. Mkataba wa mkali huyo utafika tamati mwisho wa msimu huu na huenda ikawa mwisho wake wa kuitumikia miamba hiyo ya Anfield.

Mo Salah alisema: "Hii ni mara yangu ya kwanza kusema nitapenda kubeba taji la Ligi Kuu England kuliko Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwanini? Kwa sababu pengine huu inaweza kuwa mara yangu ya mwisho kushangilia hilo nikiwa hapa. Hivyo utahitaji kufanya kitu spesho."