Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kichupa cha kipa Pickford kina balaa

KICHUPA Pict

Muktasari:

  • Kipa huyo wa Everton alicheza kwa kiwango bora kabisa wakati timu yake ilipoichapa Brighton 2-0 Jumapili iliyopita.

LONDON, ENGLAND: PICHA za uwanjani zimenasa chupa ya maji ya kipa Jordan Pickford, ambayo ameweka maelezo ya wachezaji wa timu pinzani jinsi wanavyopiga penalti zao ili kuzidaka kama alivyofanya dhidi ya mkwaju wa Danny Welbeck.

Kipa huyo wa Everton alicheza kwa kiwango bora kabisa wakati timu yake ilipoichapa Brighton 2-0 Jumapili iliyopita.

Mabao ya Iliman Ndiaye na James Garner yalitosha kuipa Everton ushindi muhimu na wa kwanza kwenye uwanja wao mpya. Mechi hiyo ilimshuhudia Jack Grealish akiasisti mabao yote mawili baada ya kujiunga na Everton kwa mkopo akitokea Manchester City dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Mashabiki wa Everton walikuwa na mashaka makubwa baada ya Brighton kupata penalti kwenye mchezo huo baada ya Kiernan Dewsbury-Hall kunawa mpira ndani ya boksi na Welbeck kutakiwa kupigwa mkwaju huo.

Lakini, kabla ya mkwaju huo kupigwa, kamera ziliivuta chupa ya maji ya Pickford kuonyesha kilichoandikwa na kipa huyo mara zote amekuwa akiweka orodha ya wachezaji wa timu pinzani na namna wanavyopiga penalti zao ili kuona ni upande gani wa kuruka.

Pickford amekuwa akitumia mbinu hiyo mara nyingi, hata alipoisaidia England kuichapa Uswisi kwenye Euro 2024. Na safari hii, kamera zilivuta jina la Welbeck kuonyesha mitindo ya upigaji wa penalti zake, ndipo ilipoonekana, staa huyo amekuwa akipiga penalti za chini kushoto na kulia. Kwenye maelezo hayo ya kwenye chupa ya Pickford ilionyesha atatakiwa kuruka upande wa kushoto ambao ni kulia kwa Welbeck.

Hilo lilionekana kuwa kweli baada ya kipa huyo kudaka mkwaju huo wa penalti ya Welbeck. Kitendo hicho kinamfanya Pickford kuingia kwenye orodha ya makipa ambao ni kiboko kwa kudaka mikwaju ya penalti.

Tangu alipojiunga na Everton mwaka 2017, Pickford amedaka penalti nane kwenye Ligi Kuu England na kuzidiwa na Lukasz Fabianski tu, ambaye amedaka penalti 10.

Na sasa Pickford anakuwa kipa namba nne Mwingereza kwa kudaka penalti nyingi, nyuma ya Rob Green na Ben Foster, ambao wamedaka penalti tisa kila mmoja, huku namba moja ni David James, aliyedaka penalti 13.