Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kante avunjiwa mkataba aende kukipiga Uturuki

KANTE Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani wa Chelsea alijiunga na klabu hiyo mwaka 2023, hatua iliyowashangaza wengi licha ya kuwa mmoja wa viungo bora wa ulinzi duniani wakati huo.

RIYADH, SAUDI ARABIA: N’GOLO Kante ameondoka kwenye klabu ya Al-Ittihad baada ya mkataba wake kuvunjwa na timu hiyo ya Ligi Kuu Saudi Arabia.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea alijiunga na klabu hiyo mwaka 2023, hatua iliyowashangaza wengi licha ya kuwa mmoja wa viungo bora wa ulinzi duniani wakati huo.

Na tangu ajiunge, Kante amecheza mechi 107, akijiunga na mastaa wakubwa kama Karim Benzema, Fabinho na Moussa Diaby.

Kante, mwenye umri wa miaka 34, alifurahia kutwaa ubingwa wa Ligi ya Saudia msimu uliopita na sasa anaondoka akiwa kileleni.

Mkataba wake na Al-Ittihad sasa umefutwa, hatua inayomfungulia njia ya kujiunga na klabu ya Uturuki, Fenerbahce.

Kante alikuwa anatarajiwa kusaini na timu hiyo ya Super Lig siku ya mwisho ya usajili baada ya pande zote kukubaliana ada ya uhamisho na mchezaji kukubaliana masharti binafsi.

Hata hivyo, kosa la kiutawala kutoka upande wa Saudia lilisababisha dili hilo kuvunjika dakika za mwisho. Youssef En-Nesyri alikuwa anatarajiwa kwenda upande wa pili kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wachezaji, lakini uhamisho wake pia ulikwama.

Mkataba wa Kante na Al-Ittihad ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu, lakini klabu hiyo imekubali kuusitisha mapema. FIFA inatarajiwa kuidhinisha uhamisho wake kwenda Fenerbahce, huku En-Nesyri tayari akitimiza uhamisho wake kwenda Al-Ittihad.

Dirisha la usajili la Ligi Kuu Uturuki (Super Lig) bado liko wazi hadi majira ya joto, lakini kwa klabu za Saudi dirisha hilo tayari limefungwa. Hilo lilimaanisha kuwa kufuta mkataba wa Kante ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuidhinisha uhamisho wake.

Fenerbahce hawakusita kueleza sababu za kuvunjika kwa dili hilo, wakilaumu Al-Ittihad moja kwa moja kupitia taarifa yao iliyosomeka: “Mchakato wa uhamisho unaohusisha N’Golo Kante na Youssef En-Nesyri na klabu ya Al-Ittihad ulifanywa kwa umakini mkubwa na kwa kufuata mipango yote iliyokubaliwa.

"Hata hivyo, kutokana na kuingizwa kimakosa kwa taarifa husika katika mfumo wa TMS na klabu pinzani, miamala haikuweza kukamilika ndani ya muda wa usajili, bila kosa lolote kutoka upande wa klabu yetu. Klabu pinzani haikukamilisha taratibu hizo bila kutupatia maelezo yoyote.”