Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kane, Diaz waiadhibu Madrid Bernabeu

Muktasari:

  • Kane, aliyekuwa akitazamwa na kocha mkuu wa England, Thomas Tuchel, alirejea uwanjani baada ya majeraha madogo yaliyomfanya kukosa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Japan pamoja na ushindi wa Bayern katika Bundesliga dhidi ya Freiburg, wikiendi iliyopita.

HARRY Kane ameonesha kurejea kwake uwanjani baada ya majeraha kwa kufunga bao la kuvutia, huku Bayern Munich ikipata faida katika robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Real Madrid kwa ushindi wa 2-1, mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa usiku wa Aprili 7, 2026 kwenye Dimba la Bernabéu, Hispania.

Kane, aliyekuwa akitazamwa na kocha mkuu wa England, Thomas Tuchel, alirejea uwanjani baada ya majeraha madogo yaliyomfanya kukosa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Japan pamoja na ushindi wa Bayern katika Bundesliga dhidi ya Freiburg, wikiendi iliyopita.

Nahodha huyo wa England mwenye umri wa miaka 32, alikuwa kimya katika kipindi cha kwanza, ingawa alihusika katika maandalizi ya bao lililofungwa na nyota  wa zamani wa Liverpool, Luis Diaz, aliyeipa Bayern uongozi kwa umaliziaji mzuri dakika nne kabla ya mapumziko.

Mara tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Kane alionyesha ubora wake kwa shuti kali la mguu wa kulia lililoingia kona ya chini ya lango, na kumuacha kipa wa Real Madrid, Andriy Lunin, bila nafasi ya kuokoa.

Kipa mkongwe wa Bayern, Manuel Neuer, alifanya sevu nne muhimu, zikiwemo tatu dhidi ya Kylian Mbappe. Hata hivyo, kikosi cha kocha Vincent Kompany kingeweza pia kufunga mabao zaidi katika mchezo uliokuwa na kasi na ushindani mkubwa.

Kwa hali ya kukata tamaa na mashabiki kuanza kuonyesha wasiwasi, Real ilimwingiza Jude Bellingham dakika ya 62 kuchukua nafasi ya Thiago Pitarch, na kiungo huyo alitoa mchango mkubwa alipokuwa uwanjani.

Trent Alexander-Arnold, ambaye alikuwa akionekana kutokuwa imara katika safu ya ulinzi, alionyesha upande mwingine wa uwezo wake kwa kutoa pasi ya chini iliyopigwa kwa ustadi na kumkuta Mbappe aliyeifungia Real Madrid bao la kufutia machozi dakika ya 74.

Real Madrid iliendelea kushambulia ikitafuta kusawazisha, lakini Bayern ilishikilia ushindi huo na kubeba faida ndogo kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa Munich, wiki ijayo.