Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juventus yahamishia nguvu kwa Silva dirisha kubwa Ulaya

Muktasari:

  • Vigogo hao wa Italia wameamua kupindukia kwa Silva baada ya kuona uwezekano wa kuipata huduma ya kiungo wa Newcastle United, Sandro Tonali, 25, ni mdogo kutokana na ushindani mkali uliopo kutoka kwa vigogo mbalimbali ambavyo pia vinahitaji saini yake ikiwemo Manchester United na Arsenal.

JUVENTUS imehamishia nguvu katika harakati za kumsajili kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva, 31, kuelekea dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi ambapo mkataba wake unatarajiwa kumalizika.

Vigogo hao wa Italia wameamua kupindukia kwa Silva baada ya kuona uwezekano wa kuipata huduma ya kiungo wa Newcastle United, Sandro Tonali, 25, ni mdogo kutokana na ushindani mkali uliopo kutoka kwa vigogo mbalimbali ambavyo pia vinahitaji saini yake ikiwemo Manchester United na Arsenal.

Silva ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu, tangu kuanza mwaka amekuwa akitajwa kuwa anaweza kuondoka Man City licha ya kwamba haijathibitishwa. Kumekuwapo na ofa pia kutoka klabu za Saudi Arabia ambazo zinamhitaji lakini mwenyewe hajaonyesha nia ya kutaka kujiunga nazo kwani bado anahitaji kuendelea kucheza soka la ushindani. Hadi sasa Silva hajafanya uamuzi wowote ingawa inaaminika kwamba anataka kusubiri hadi michuano ijayo ya Kombe la Dunia itakapomalizika.


Leon Goretzka

ARSENAL huenda ikaangukia pua katika mbio za kumsajili kiungo wa kimataifa wa Bayern Munich na Ujerumani, Leon Goretzka, 31, kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya Juventus nayo kuingia katika mbio hizo. Goretzka anatarajiwa kuondoka Bayern mwishoni mwa msimu huu ambapo mkataba wake utakuwa unamalizika, jambo ambalo limevutia vigogo kadhaa Ulaya. Inaelezwa Arsenal na Juventus zote zinaona ni fursa kubwa kumsajili.


Said El Mala

BRIGHTON ina nia ya kukamilisha haraka dili la kumsajili winga chipukizi wa FC Koln ya Ujerumani, Said El Mala, 19. Inaelezwa kuwa mazungumzo yamepata kasi baada ya mchezaji huyo kubadilisha mawakala wake, hatua inayotafsiriwa kuwa ni ishara ya kuwa tayari kwa uhamisho mpya. Brighton inaendelea na mkakati wake wa kusajili vipaji changa barani Ulaya, na El Mala anaonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoweza kung’ara siku za usoni.


Adam Wharton

KOCHA Xabi Alonso anatajwa kuwa na mipango maalumu ya usajili iwapo atachukua mikoba ya Arne Slot katika kikiosi cha Liverpool msimu ujao na miongoni mwa mastaa ambao anadaiwa kutaka wasajiliwe ni beki wa Inter Milan, Alessandro Bastoni, 26; kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton, 22 pamoja na winga wa PSG, Bradley Barcola, 23. Majina hayo yanaripotiwa kuwa yamewasilishwa kama sehemu ya mpango kazi.


Savinho

MANCHESTER City inaweza kumruhusu winga wa kimataifa wa Brazil, Savinho, 21, kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kusajili mtu mwingine bora. Inaelezwa kwamba Tottenham Hotspur ni miongoni mwa timu zinazohitaji sana huduma yake na kwa sasa inafanya mazungumzo na wawakilishi wake kujua kama staa huyo atakuwa tayari kujiunga kwa msimu ujao. Savinho anakumbana na ushindani Man City.


Mika Godts

MANCHESTER United imeanza mawasiliano na Ajax kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji chipukizi wa klabu hiyo na Ubelgiji, Mika Godts, 20. Inaelezwa kuwa mazungumzo hayo yapo katika hatua ya awali ambapo Man United imeomba kujulishwa ada ya uhamisho ambayo Ajax inaitaka na masharti mengine ya mauziano. Godts anatajwa kuwa miongoni mwa mastaa wenye vipaji vikubwa  Ulaya na maskauti wa timu nyingi.


Kees Smit

VIGOGO wa Hispania, Real Madrid na Barcelona wanaongoza mbio za kumsajili kiungo chipukizi wa kimataifa wa Uholanzi, Kees Smit, 20, kutoka AZ Alkmaar. Inaelezwa klabu hizo ziko mbele ya timu za Ligi Kuu England katika vita hiyo na sababu kubwa inatajwa ni mchezaji kutamani zaidi kwenda Hispania kuliko taifa lolote Ulaya. Smit amechagua huko kutokana na hali nzuri ya hewa.


Joao Gomes

LIVERPOOL na Manchester United zinapigana vikumbo kuwania saini ya kiungo wa Wolves, Joao Gomes, 25. Inaelezwa kuwa timu hizo zina uhitaji wa kuboresha maeneo ya kiungo na zinaona Gomes ni mmoja kati ya mastaa wanaoonekana kuvutiaa. Inaelezwa Gomes anafikiria kuondoka Wolves mwisho wa msimu huu ambapo kwa zaidi ya asilimia 70 timu yake inakwenda kushuka na hataki kucheza Daraja la Kwanza.