Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jurgen Klopp atoa neno dili la Real Madrid

KLOPP

Muktasari:

  • Madrid ilimfukuza kocha wao, Xabi Alonso, mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kudumu kwa miezi minane kasoro na kushindwa kufikia malengo.

MADRID, HISPANIA: IMEFICHUKA! kocha Jurgen Klopp ameweka wazi hataki kwenda Madrid hata timu hiyo ikiwasilisha ofa mzani kwa sasa.

Madrid ilimfukuza kocha wao, Xabi Alonso, mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kudumu kwa miezi minane kasoro na kushindwa kufikia malengo.

Baada ya kuondoka, Madrid ilimteua mchezaji wao mwingine wa zamani, Alvaro Arbeloa aliyekuwa akifundisha kikosi chao cha vijana kabla ya hapo.

Kazi yake ilianza vibaya baada ya Madrid kutolewa kwenye Kombe la Copa del Rey katika raundi ya tatu na Albacete ya daraja la pili.

KLO 01

Hata hivyo, Madrid ilirejea kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Levante kwenye La Liga, kisha kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Monaco kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Maelezo kuhusu uteuzi wa Arbeloa bado yana ukakasi ikiwa haijaeleweka kama ni kocha wa muda tu au ndio moja kwa moja jambo linalozua  tetesi za wababe hao kuwa na mpango wa kuajiri kocha mwingine mwisho wa msimu.

Gazeti la Diario AS limeripoti jina la kocha wa zamani wa Liverpool, Klopp, lilitajwa na viongozi wa Madrid mwanzoni mwa mwezi huu kama mtu anayepaswa kuchukua mikoba ya kuifundisha timu hiyo.

Kocha huyo Mjerumani kwa sasa anafanya kazi kama Mkuu wa Masuala ya soka Duniani katika kampuni ya Red Bull na alipoulizwa kuhusu tetesi za kutakiwa na Madrid na tovuti ya The Athletic, Klopp alikiri amesema: "Nafurahia kusikia tetesi hizo, inaonyesha watu wanajali kuhusu mimi, pia sipendezwi nazo sana. Ninajua ninaweza kufundisha timu yoyote  ya soka, lakini hiyo si ishara kuwa lazima nifanye hivyo hadi siku yangu ya mwisho… Kwa sasa sitaki kufundisha timu yoyote."

KLO 02

Hata hivyo, kituo cha habari cha Madrid, Defensa Central kilisema iwapo Klopp angeulizwa na Madrid na kuamua kukubali kazi hiyo, angependa kuuza wachezaji wawili.

Inadaiwa mabeki wa pembeni, Daniel Carvajal na Ferland Mendy, wangekuwa wachezaji wa kwanza kuondoka kama sehemu ya mpango wa Klopp wa ujenzi upya.

Carvajal ana ushindani wa moja kwa moja kwa nafasi ya beki wa kulia na Trent Alexander-Arnold, ambaye Klopp alimuendeleza mmoja wa mabeki wa bora duniani akiwa Liverpool. Vilevile Mendy haonekani kuendana na mfumo wa kocha huyo.