Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jurgen Klopp atamani kurudi mzigoni

KLOPP Pict

Muktasari:

  • Klopp, mwenye umri wa miaka 58, hajafundisha tangu Mei 2024 baada ya kumaliza kipindi cha mafanikio cha miaka tisa akiwa kocha wa Liverpool na aliondoka akisema alikuwa amechoka na anahitaji mapumziko.

MUNICH, UJERUMANI: KOCHA wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp anaweza kufanya uamuzi wa kushangaza na kurejea tena kufundisha soka baada ya kuanza kuhisi hamu ya kurudi kwenye benchi la ufundi.

Klopp, mwenye umri wa miaka 58, hajafundisha tangu Mei 2024 baada ya kumaliza kipindi cha mafanikio cha miaka tisa akiwa kocha wa Liverpool na aliondoka akisema alikuwa amechoka na anahitaji mapumziko.

Baadaye, Januari 2025, kocha huyo Mjerumani alichukua nafasi ya Mkuu wa Soka Duniani katika kampuni ya Red Bull, akisimamia timu zote za soka zilizo chini ya kundi hilo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Sky Sports, Klopp sasa anaonyesha dalili za kutaka kurejea tena kufundisha. Klopp, aliyewahi pia kuinoa Borussia Dortmund bado anahusishwa na kazi mbili kubwa, Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani.

Kwa upande wa Real Madrid, klabu hiyo kwa sasa imemweka Alvaro Arbeloa kama kocha wa muda baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wao Xabi Alonso, Januari. Real Madrid inaendelea kumfuatilia Klopp, ingawa hadi sasa hakuna mazungumzo rasmi yaliyofanyika.

Inaelezwa Real Madrid ndiyo klabu pekee inayoweza kumshawishi Klopp kubadilisha uamuzi wake na kurejea tena kufundisha soka la klabu.

Hata hivyo, miamba hiyo ya Hispania haitarajiwi kufanya uamuzi kuhusu kocha mpya kabla ya mwisho wa msimu huu.

Kwa upande mwingine, timu ya taifa ya Ujerumani pia ni chaguo jingine linalowezekana, huku viongozi wa soka nchini humo wakiendelea kufuatilia hali yake. Lakini, Ujerumani itaanza kutafuta kocha mpya tu ikiwa kocha wa sasa Julian Nagelsmann atashindwa kufanya vizuri katika Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika baadaye mwaka huu huko Marekani, Mexico na Canada.