Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jurgen Klopp amfuta kazi kocha mwingine

KLOPP Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo wa zamani wa Liverpool, Klopp, ambaye sasa anasimamia klabu zote zilivyo chini ya mtandao wa Red Bull ikiwemo Paris FC, amechukua uamuzi wa kumfuta kazi kocha wa klabu hiyo ya Ufaransa ikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligue 1.

MUNICH, UJERUMANI: JURGEN Klopp amefanya uamuzi mwingine mzito kwa mara ya pili ndani ya wiki moja katika nafasi yake mpya kama mkuu wa soka wa kimataifa wa kampuni ya Red Bull GmbH baada ya kumfuta kazi kocha mwingine.

Kocha huyo wa zamani wa Liverpool, Klopp, ambaye sasa anasimamia klabu zote zilivyo chini ya mtandao wa Red Bull ikiwemo Paris FC, amechukua uamuzi wa kumfuta kazi kocha wa klabu hiyo ya Ufaransa ikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligue 1.

Kocha wa Paris FC, Stephane Gilli, ndiye meneja wa hivi karibuni kuondolewa na Klopp.

Hatua hiyo imekuja licha ya Klopp kumtetea hadharani Gilli katika mahojiano ya hivi karibuni wakati presha ilipokuwa ikiongezeka juu ya Mfaransa huyo, akisisitiza anaamini katika mradi huo na kiongozi wake.

Lakini, huku lengo kuu la klabu likiwa ni kubaki Ligue 1 msimu huu, viongozi wa Red Bull wameamua kuchukua hatua.

Taarifa ya klabu iliyotolewa Jumapili ilithibitisha uamuzi huo, ikisema: “Paris FC inatangaza kusitisha ushirikiano wake na Stephane Gilli, kocha wa timu ya kwanza, kuanzia Februari 22, 2026. Baada ya kuchukua jukumu la kocha mkuu mwaka 2023, Stephane ameacha alama kubwa katika klabu. Katika misimu miwili, amechangia mafanikio mengi ya timu, yakihitimishwa na kurejea kwa Paris FC katika Ligue 1, hatua muhimu katika historia ya hivi karibuni ya klabu.

“Klabu inapenda kumshukuru kwa dhati Stephane Gilli kwa kujitolea kwake, weledi wake na kazi yote aliyoifanya akiwa Paris FC. Stephane Gilli atabaki katika kumbukumbu za wote wanaoipenda klabu hii, aliyeruhusu irejee Ligue 1 karibu nusu karne baada ya kuondoka. Uadilifu wa hali ya juu wa kitaaluma, bidii isiyochoka, uaminifu na wema wake uliothaminiwa na wote vitaendelea kukumbukwa. Nina imani kuwa kipaji na uwezo wake vitaendelea kuonekana katika viwango vya juu zaidi. Paris FC inamtakia kila la heri katika hatua inayofuata ya taaluma yake.”

Gilli aliiongoza klabu kurejea Ligi Kuu katika mafanikio yaliyotajwa kuwa ya kihistoria. Lakini, kutokana na matokeo kushuka na hofu ya kushuka daraja kuongezeka, Klopp pamoja na uongozi wa Red Bull wameamua kufanya mabadiliko.

Huyu ni kocha wa pili kuondolewa kwa muda mfupi chini ya usimamizi wa Klopp. Mapema wiki iliyopita, Thomas Letsch alifutwa kazi katika kikosi cha Red Bull Salzburg. Letsch alichukua mikoba mwanzoni mwa mwaka 2025 na alidumu kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuondolewa. Wajibu wa kiutendaji wa Klopp unamhusisha kusimamia mtandao mzima wa klabu vya Red Bull, akifanya maamuzi muhimu ya kimkakati na kisoka, ikiwemo uteuzi wa makocha.