Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jules Kounde hana furaha Barcelona

KOUNDE Pict

Muktasari:

  • Baada ya kusherehekea mataji ya La Liga na Supercopa de Espana msimu huu katika mitaa ya Barcelona wiki iliyopita, kikosi cha Barcelona kilihitimisha msimu kwa chakula maalumu kilichowakutanisha wachezaji, wenzi wao, benchi la ufundi pamoja na viongozi wa juu wa klabu hiyo.

BARCELONA, HISPANIA: BEKI mahiri wa kulia wa Barcelona, Jules Kounde huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu ikielezwa hana furaha katika kikosi hicho chini ya Kocha Hans Flicki wengi katika nafasi ya beki wa kulia, wakiwemo Eric García, Xavi Espart, Joao Cancelo, Hector Fort (anayekipiga kwa mkopo Elche) pamoja na Ronald Araujo.

Baada ya kusherehekea mataji ya La Liga na Supercopa de Espana msimu huu katika mitaa ya Barcelona wiki iliyopita, kikosi cha Barcelona kilihitimisha msimu kwa chakula maalumu kilichowakutanisha wachezaji, wenzi wao, benchi la ufundi pamoja na viongozi wa juu wa klabu hiyo.

Hata hivyo, wakati hafla ya chakula hicho cha usiku, tukio lililovuta hisia za wengi ni Kounde kuondoka mapema katika Klabu ya Casanova Beach, jambo lililoongeza uvumi kuhusu uwezekano wa kuondoka kwake.

KOUND 01

Kama alivyoeleza mwandishi mahiri wa habari za uchunguzi za michezo Hispania, Jose Alvarez, Kounde anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa watakaoondoka Barcelona kwa kuwa hafurahii maisha kikosini licha ya kwamba ana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.

“Chakula kilianza saa 3:00 usiku na yeye aliondoka saa 3:47 usiku, wakati wimbo wa Barcelona ukiwa unapigwa mara tu baada ya hotuba ya Joan Laporta aliondoka. Kwa maneno mengine alikula ‘apetaiza’ pekee,” alisema Alvarez na kuongeza:

“Jina lake ni Jules Kounde, na nadhani anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wanaoondoka Barcelona.”

KOUND 02

Tangu kuwasili kwake kutoka Sevilla 2022, mchezaji huyo amekuwa mchezaji muhimu na anachukuliwa kuwa mmoja wa mabeki bora wa kulia duniani. Ingawa kiwango chake kilipungua msimu huu, lakini thamani yake sokoni bado ipo juu na Barcelona inaweza kutumia hilo kupata fedha nyingi katika mauzo yake.

Habari hizo zinakuja wakati Barcelona ikiendelea kuimarisha hali yake ya kifedha na katika madirisha matatu ya usajili yaliyopita viongozi wa klabu walilazimika kuwaacha baadhi ya wachezaji muhimu ili kuweka sawa hesabu za fedha na kusajili wachezaji wapya.

Barcelona ina wachezaji wengi katika nafasi ya beki wa kulia, wakiwemo Eric García, Xavi Espart, Joao Cancelo, Hector Fort (anayekipiga kwa mkopo Elche) pamoja na Ronald Araujo.