Jose Mourinho haishiwi vituko
![](/resource/image/4885704/landscape_ratio2x1/320/160/4d61e434faac46ca816466ca53aae654/FN/morihno-pc.jpg)
Muktasari:
- Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Manchester United na Tottenham alikiongoza kikosi chake cha Fenerbahce kukabiliana na Kasimpasa na kushinda 3-0
ISTANBUL, UTURUKI: JOSE Mourinho ana vituko sana. Hicho ndicho unachoweza kusema baada ya kocha huyo kwenda kuzungumza na wachezaji wa timu pinzani akiwaelekeza jambo baada ya kuwafunga katika mchezo wa Kombe la Uturuki.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Manchester United na Tottenham alikiongoza kikosi chake cha Fenerbahce kukabiliana na Kasimpasa na kushinda 3-0
Baada ya mechi, Mourinho aliwakusanya wachezaji wa Kasimpasa ambao ilikuwa na vijana wengi na kuanza kuwapa somo. Tukio hilo liliwavutia wengi kwa sababu Mourinho alipomaliza kuzungumza na wachezaji hao wa timu pinzani walimpigia makofi.
Baada ya tukio hilo kufika kwenye mitandao ya kijamii, shabiki mmoja aliandika: “Anapenda soka. Anataka kuwahamasisha vijana.”