Jina la Højlund lazua utata

MANCHESTER, ENGLAND. MADUKA ya kuuza jezi ya klabu ya Manchester United yalishindwa kuuza jezi ya mchezaji mpya Rasmus Højlund kwa sababu jina lake la pili haikuwa na herufu ‘øs’ iliyoandikwa kwa lugha ya Denmark.

Mashabiki walikuja juu baada ya kuambiwa kwamba maduka yote ya Megastore kutoka Old Trafford walikuwa wanasubiri ujio wa herufi hiyo ya jina lake pili.

Højlund aliyejiunga na Man United akitokea Atalanta kwa Pauni 72 milioni jezi zake hazikuwekwa sokoni huku mshabiki waliojaribu kununua jezi ya straika huyo wakiambiwa wasubiri hadi ujio wa herufi ø halafu klabu itatoa taarifa rasmi.

Aidha mashabiki wameikosoa klabu yao wakidai uongozi wa klabu haupo siriazi katika masuala ya mbalimbali nje na ndani ya uwanja.

Shabiki mmoja alizungumzia kuhusu uzembe wa klabu yao akisema: "Man United imeshindwa kutengeneza jina la jezi ya mchezaji mpya aliyesajiliwa, kwa sababu hakuna mtu aliyeweza kuipata herufi ‘øs’."

Wakati huo huo kwa mujibu wa ripoti Man United iliripoti kwamba herufi ‘øs’ iliwasili Alhamisi na tayari jezi ya straika huyo zimeanza kuuzwa madukani.