Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jesus afunguka mpango wake wa kurejea Palmeiras

Muktasari:

  • Hata hivyo, Mbrazili huyo alisema hana mpango wa kuachana na Arsenal kwa sasa, ambapo alijiunga na timu hiyo akitokea Manchester City mwaka 2022.

LONDON, ENGLAND: GABRIEL Jesus amefichua dhamira yake ya kurudi kwenye timu yake ya zamani Palmeiras wakati atakapoamua kuachana na Arsenal.

Hata hivyo, Mbrazili huyo alisema hana mpango wa kuachana na Arsenal kwa sasa, ambapo alijiunga na timu hiyo akitokea Manchester City mwaka 2022.

Arsenal ililipa Pauni 45 milioni kunasa huduma ya Jesus, lakini bahati mbaya mchezaji huyo amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara yaliyomfanya awe ameitumikia timu hiyo mechi 96 tu na kufunga mabao 26.

Jesus mara kwa mara amekuwa akihusishwa na mpango wa kuachana na Arsenal, ambapo Everton ilidaiwa kuhitaji huduma yake kwa kipindi cha hivi karibuni, lakini miamba hiyo ya Emirates haitakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo kwa wapinzani ndani ya Ligi Kuu England.

Jesus, 28, mwenyewe alifunguka juu ya hatima yake, akibainisha mpango wa kurudi Palmeiras pale muda mwafaka utakapowadia, akisema: “Sijawahi kuwasiliana na klabu nyingine na mipango yangu ipo wazi, kurudi Palmeiras na Palmeiras ndoto zake kwangu ni kurudi Palmeiras.

“Wakati nitakapoona ni muda wa kurudi Palmeiras, nitajadili hilo la Arsenal, lakini hapa tunamzungumzia mchezaji ambaye yupo nje kwa miezi tisa na anapambana kurudi kwenye timu.”

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alisema juu ya hatima ya Jesus huku akibainisha wazi dhamira yake ya kumtaka Mbrazili huyo kuendelea kubaki kwenye kikosi chake, akisema: “Ni mchezaji asiyetabirika, ana nguvu, mshindani ni mchezaji ambaye anaweza kupambana na mambo magumu kama ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu. Kwa kiwango chake cha njaa ya mafanikio alichonacho, hicho ndicho kitu tunachokitaka, kwa sababu ataleta kitu kwenye timu.”

Jesus alianzia soka lake la kulipwa huko Palmeiras, akifunga mabao 28 katika mechi 83 kabla ya kunaswa na Man City kwa ada ya Pauni 27 milioni. Fowadi huyo aliisaidia Man City kubeba mataji manne ya Ligi Kuu England, Kombe la FA na mataji matatu ya Kombe la Ligi, akifunga mabao 95 katika mechi 236 katika michuano yote.