Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jeremie Frimpong akaribia kumalizana na Liverpool

Muktasari:

  • Frimpong anasajiliwa kwa ajili ya kwenda kuziba pengo la Trent Alexander Arnold anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

BEKI wa kulia wa Uholanzi na klabu ya Bayer Leverkusen, Jeremie Frimpong, 24, yuko karibu kuhamia Liverpool kwa ada ya Pauni 29.5 milioni katika dirisha lijalo la usajili ikidaiwa kuwa tayari ameshafanya hadi makubaliano binafsi kwa ajili ya kutua Anfield.

Frimpong anasajiliwa kwa ajili ya kwenda kuziba pengo la Trent Alexander Arnold anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Benchi la ufundi la Liverpool limevutiwa sana na staa huyu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga na kutoa asisti za mabao aliouonyesha tangu msimu uliopita akiwa na Leverkusen.

Staa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu huu amecheza mechi 48 za michuano yote, amefunga mabao matano na kutoa asisti 12.


Liam Delap

MANCHESTER United iko katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Ipswich Town na timu ya taifa ya England, Liam Delap, mwenye umri wa miaka 22, ambaye amewaeleza watu wake wa karibu kwamba angetamani sana kutua Old Trafford katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mkataba wa sasa wa Delap na Ipswich unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote na kufunga mabao 12.


James McAtee

NOTTINGHAM Forest inapanga kusajili wachezaji wasiopungua watano katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa pamoja na kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya England, James McAtee, mwenye umri wa miaka 22.

Bosi wa timu hii anataka kufanya usajili wa kutosha katika dirisha lijalo ili kuonyesha ushindani zaidi katika michuano ya kimataifa kwa msimu ujao ambayo wameshafuzu.


Dean Huijsen

ARSENAL na Liverpool zinatamani sana kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 20, Dean Huijsen, anayeichezea Bournemouth.

Beki huyu anadaiwa kuhitaji zaidi kutua Madrid kuliko timu nyingine yoyote na tayari vigogo hao wameshaanza mchakato wa kutaka kumsajili.

Bournemouth inahitaji Pauni 50 milioni ili kumuuza.



Trent Alexander-Arnold

REAL Madrid wako karibu kutangaza usajili wa beki wa kulia wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Trent Alexander-Arnold, 26, ambaye ripoti zinadai Madrid ipo tayari kutoa Pauni 840,000 kama ada ya uhamisho ili kuweza kumtumia katika michuano ya Kombe la Dunia la Klabu ambayo wakati inaanza mkataba wake na Liverpool utakuwa bado haujamalizika.



James Milner

BRIGHTON iko kwenye mazungumzo na kiungo wake mkongwe raia wa England, James Milner, 39, kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia.

Vigogo wa Brighton wanatamani sana staa huyu aongeze mkataba mpya kutokana na mchango wake licha ya kutokuwa chaguo la kwanza la kocha. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu.


Antoine Semenyo

MANCHESTER United imefanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, mwenye umri wa miaka 25, kuhusu uwezekano wa kumpata katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mkataba wake unamalizika mwaka 2029. Msimu huu amecheza mechi 40 za michuano yote.


Jonathan Tah

BEKI wa kati wa Bayer Leverkusen, Jonathan Tah, 29, anadaiwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kutua Barcelona katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya mwenyewe hivi karibuni kusisitiza kwamba hadi sasa bado hajafanya uamuzi wa timu gani atajiunga nayo. Staa huyu wa kimataifa wa Ujerumani mkataba wake na Leverkusen unamalizika msimu huu.