Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

England yapewa shavu kombe la dunia

ENGLAND Pict

Muktasari:

  • England haijawahi kuwania kuandaa Kombe la Dunia tangu kura ya utata ya mwaka 2010 kuhusu mashindano ya 2018 na 2022 yaliyopewa Urusi na Qatar na ilidaiwa baadhi ya wajumbe wa Fifa walihongwa kupigia kura mataifa hayo kuwa wenyeji.

LONDON, ENGLAND: ENGLAND huenda ikaandaa Kombe la Dunia baada ya kusubiri kwa miaka 70, kutokana na kauli ya kiongozi wa juu wa Fifa kuhamasisha nchi hiyo kuwania uenyeji wa mashindano hayo.

England haijawahi kuwania kuandaa Kombe la Dunia tangu kura ya utata ya mwaka 2010 kuhusu mashindano ya 2018 na 2022 yaliyopewa Urusi na Qatar na ilidaiwa baadhi ya wajumbe wa Fifa walihongwa kupigia kura mataifa hayo kuwa wenyeji.

England haijawahi kuandaa Kombe la Dunia tangu lile la kihistoria la mwaka 1966 na kikosi cha Sir Alf Ramsey kilishinda taji hilo.

Makamu wa rais wa Fifa, Victor Montagliani anaamini ni wakati mwafaka kwa mashindano hayo kurejea nchini humo.

Akizungumza na gazeti la The Times, alisema: “Siwezi kuona sababu kwa nini, si tu England bali Uingereza kwa jumla, wasiwe wenyeji wa Kombe la Dunia. Nadhani litakuwa Kombe la Dunia la kuvutia sana na wanapaswa kufikiria kwa umakini na kuwasilisha ombi lao.”

“Sote tunajua mchezo huu unavyothaminiwa Uingereza na nadhani muda umefika.”

Kombe la Dunia la 2026 litafanyika Marekani, Canada na Mexico, wakati lile la 2030 litagawanywa kati ya Hispania, Ureno, Morocco na mataifa ya Amerika Kusini.

Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa mashindano ya 2034 baada ya kukosa wapinzani katika kinyang’anyiro cha kuwania uenyeji wa kuandaa mwaka huo.

Kombe la Dunia la Wanawake litafanyika Uingereza mwaka 2035 na linaweza kuwa kichocheo cha kurudisha Kombe la Dunia la wanaume nchini humo mwaka 2038 au 2042.

Akizungumzia mfumo wa mzunguko wa uenyeji wa Fifa, Montagliani alisema:

Kombe la Dunia la mwakani litakuwa la kwanza kushirikisha timu 48. Hata hivyo, viongozi wa soka wa Amerika Kusini wamependekeza mashindano yajayo yaongezwe hadi timu 64 jambo ambalo Montagliani anaamini litapunguza hadhi ya kufuzu kwenye mashindano hayo.

“Timu 64 ni nyingi mno kwa maoni yangu. Hatujaanza hata kucheza kwa mfumo wa timu 48, ingawa nadhani tutaweza kuumudu,” alisema Montagliani.

“Tulipo sasa ni sawa na siungi mkono kuongeza zaidi, kuwa na timu chache  bado ni muhimu. Bado inapaswa kuwa ngumu kufuzu Kombe la Dunia, na kwa timu 48 bado kutakuwa na baadhi ya mataifa yanayostahili lakini yatashindwa kufuzu.”