Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jeraha la Isak, Slot atoa neno

SLOT Pict

Muktasari:

  • Isak alilazimika kutolewa uwanjani katika mechi dhidi ya Tottenham iliyomalizika kwa Liverpool kushinda mabao 2-1.

LIVERPOOL, ENGLAND: BAADA ya sintofahamu kuhusu majeraha ya straika wa Liverpool, Alexander Isak, kocha wa timu hiyo Arne Slot amesema timu ya madaktari itatathmini ukubwa wa jeraha lake na kutoa taarifa zaidi.

Isak alilazimika kutolewa uwanjani katika mechi dhidi ya Tottenham iliyomalizika kwa Liverpool kushinda mabao 2-1.

Staa huyu aliondolewa uwanjani dakika 10 tu baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba kipindi cha pili, baada ya kugongwa vibaya na Micky van de Ven wakati anafunga bao.

Fundi huyu wa kimataifa wa Sweden aliyesajiliwa katika dirisha la majira ya kiangazi kwa Pauni 125 milioni, licha ya kucheza kwa muda mchache, aliipa Liverpool bao la kuongoza kwa shuti lililompita kipa Guglielmo Vicario.

Hata hivyo, hakufurahia bao hilo kwani Van de Ven alimchezea vibaya wakati akijaribu kumzuia asipige shuti hilo.

Isak alionekana kuwa katika maumivu makali, huku wachezaji wenzake wakimzunguka kwa wasiwasi na haraka alisaidiwa kutoka uwanjani na madaktari wa Liverpool na nafasi yake ikachukuliwa na Jeremie Frimpong.

"Tusubiri tuone," Slot aliambia BBC Match of the Day alipoulizwa kuhusu hali ya Isak. "Ni mapema sana kuzungumzia suala hilo, lakini haonekani kuwa katika hali nzuri ndio maana alilazimika kutolewa nje. Kuhusu Frimpong yuko sawa. Wengine wawili Isak na Conor Bradley kwakweli tutalazimika kusubiri tuone. Jambo jema ni kwamba tuna wiki moja, hivyo tunatumaini tutakuwa na wachezaji wa kutosha kwa ajili ya mechi ya wiki ijayo.

"Sina taarifa zozote za ziada kuhusu Isak, lakini nikiri kwamba ameumia, ukiona mchezaji anafunga bao na anashindwa kabisa kuendelea ujue ni jambo baya limemtokea, ni sawa na ilivyokuwa kwa Conor Bradley ambaye alijaribu kutaka kurudi, lakini nililazimika kumtoa kwa sababu hakuweza kuendelea."