Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot: Mo Salah baada ya AFCON 2025

SLOT Pict

Muktasari:

  • Ekitike alifungua ukurasa wa mabao katika mechi hiyo kwa shuti safi la sekunde ya 46 tu tangu kuanza kwa mechi, ambalo lilikuwa ni bao la mapema zaidi la Liverpool kwenye Ligi Kuu tangu lile la Naby Keita dhidi ya Huddersfield Aprili 2019.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot anatarajia mshambuliaji wa timu hiyo Mohamed Salah kubakia katika kikosi chao hadi mwisho wa msimu.

Salah aliingia akitokea benchini kuisaidia Liverpool kupata ushindi mbele ya Brighton, ikiwa ni wiki moja baada ya kueleza kwamba huenda asicheze tena akidai kwamba timu haimpi heshima anayostahili na kuna watu wanataka kumwangushia jumba bovu.

Jina la mshambuliaji huyo liliimbwa na mashabiki wa Liverpool baada ya mechi dhidi ya Brighton kumalizika, alipokuwa akiwapungia mkono kuaga kabla ya kuondoka kwenda kuitumikia Misri kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Slot, ambaye alifanya mazungumzo ya ana kwa ana na Salah Ijumaa, amesema: “Ninatarajia atarejea baada ya AFCON.

SLO 01

“Ilikuwa uamuzi rahisi kumjumuisha kwenye kikosi. Nilikuwa nimeridhika na kile tulichozungumza mimi na yeye, la sivyo nisingefanya hivyo. Kilichozungumzwa kati yetu katika mazungumzo hayo kitabaki kati yetu. Kile unachokiona ndicho unachopaswa kujua ambacho ni kwamba alikuwa kwenye kikosi  na alikuwa mchezaji wa kwanza kumfanyia mabadiliko.”

Salah mwenye umri wa miaka 33, amesema  kuwa ni kama Liverpool ilikuwa “imemtupa chiniya basi” baada ya kuendelea kuwekwa benchini katika mechi kadhaa.

Pia alieleza kwamba uhusiano wake na kocha Slot ulikuwa umeharibika na baada ya hapo, aliachwa nje ya kikosi cha Liverpool kilichosafiri kwenda Italia kucheza dhidi ya Inter Milan katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Salah alianza mechi ya Jumamosi dhidi ya Brighton akiwa benchini kwa mara ya nne mfululizo tangu Slot, raia wa Uholanzi, achukue mikoba ya kuinoa timu hiyo msimu uliopita.

SLO 02

Hata hivyo, alikuwa na mchango mkubwa katika mechi hiyo, akipiga mpira wa kona uliomkuta Hugo Ekitike aliyefunga bao lake la pili la siku hiyo kwenye Uwanja wa Anfield.

Pasi hiyo ya bao ilimfanya Salah avunje rekodi nyingine, ahuihusike katika mabao mabao 277 ya kwenye Ligi Kuu England na hiyo ilimfanya kuvunja rekodi ya Wayne Rooney aliyoweka akiwa Manchester United.

Baada ya bao hilo, Salah alionekana mwenye furaha kama ilivyokuwa kwa kocha wake Slot, huku Liverpool ikifikisha mechi tano bila kupoteza katika mashindano yote.

 Kabla ya hapo, Majogoo hao walikuwa wamepoteza mechi tisa kati ya 12 za michuano yote.

“Sababu ya yeye kutokuwapo Milan ilikuwa ni mahojiano yake. Nilizungumza naye jana na alipoingia kama  mchezaji wa akiba, alifanya kile ambacho kila mtu angependa kukiona. Mo ataenda AFCON, ninatumai atafanya vizuri sana.”

Ekitike alifungua ukurasa wa mabao katika mechi hiyo kwa shuti safi la sekunde ya 46 tu tangu kuanza kwa mechi, ambalo lilikuwa ni bao la mapema zaidi la Liverpool kwenye Ligi Kuu tangu lile la Naby Keita dhidi ya Huddersfield Aprili 2019.