James Milner akubali yaishe, ajiweka pembeni
Muktasari:
- Milner, ambaye mwezi Februari aliweka rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi ya Ligi Kuu, amemaliza taaluma yake akiwa na jumla ya michezo 658.
LONDON, ENGLAND: James Milner, kiungo wa Brighton, Liverpool na Manchester City, amethibitisha kustaafu soka rasmi akiwa na umri wa miaka 40, akiwa ametumika kwenye Ligi Kuu England kwa misimu 24.
Milner, ambaye mwezi Februari aliweka rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi ya Ligi Kuu, amemaliza taaluma yake akiwa na jumla ya michezo 658.
Alitumia miaka mitatu ya mwisho ya taaluma yake akiwa na Brighton na kuisaidia klabu hiyo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Conference League msimu ujao.
“Baada ya misimu 24 katika Ligi Kuu, sasa ni wakati muafaka kumalizia muda wangu wa uchezaji,” Milner aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram. “Kuanzia nilipoanzia Leeds United, klabu niliyokuwa nikipenda toka moyoni, nikiwa mtoto wa miaka 16 na kuwa mfungaji mdogo zaidi katika historia ya Ligi Kuu, siwezi kufikiria safari hii niliyoipitia, hadi kushindwa kuinua mguu mwaka jana kisha kurudi kusaidia Brighton kufuzu michuano ya Ulaya mara ya pili katika historia yao nikiwa na miaka 40.”
Milner alianza kucheza Leeds United akiwa na miaka 16 na kuwa mchezaji wa pili mdogo zaidi kucheza Ligi Kuu wakati huo. Baada ya mkopo wa muda mfupi Swindon Town, aliichezea Newcastle United chini ya Sir Bobby Robson kabla ya kwenda Aston Villa, ambapo kiwango chake lilimfanya aweze kujiunga na Manchester City chini ya kocha Roberto Mancini.
Alitwaa mataji mawili ya Ligi Kuu, FA Cup na League Cup na Man City kabla ya kuhamia Liverpool mwaka 2015 kwa usajili wa bure hatua ambayo inachukuliwa kuwa moja ya mikataba bora zaidi katika historia ya soka.
Liverpool, chini ya Jurgen Klopp, ilifaidika sana na Milner. Alijulikana kwa uthabiti wake na uwezo wa kucheza nafasi nyingi, na kumchangia klabu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya la sita msimu wa 2018/19, pamoja na kutwaa Premier League baada ya kupita kwa miaka 30. Pia alichangia ushindi wa Club World Cup, League Cup na FA Cup.
Milner pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England tayari ana makombe 61 kabla ya kustaafu kimataifa mwaka 2016.
“Kuichezea Newcastle, Aston Villa, Man City, Liverpool na Brightonna pia kukaa kipindi kifupi kilisichosahaulika Swindon Town, imekuwa heshima kubwa. Kila klabu imekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu na taaluma yangu,” Milner aliongeza.
“Nilikuwa na bahati ya kushuhudia matukio yasiyosahaulika, kushinda mataji, kucheza Ulaya, na kuwakilisha nchi yangu katika Michuano ya Ulaya na Kombe la Dunia mara mbili. Lakini zaidi ya yote, ni watu na urafiki niliyojenga katika soka nitakavyoyathamini milele amesema beki huyo mahiri.”