Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ivory Coast mabingwa wa Afrika 2015

Muktasari:

Mabingwa wapya wa Afrika, Ivory Coast walifunga penalti zao kupitia kwa Serge Aurier, Seydou Doumbia, Yaya Toure, Salomon Kalou, Kolo Toure, Kanon, Serey Die na Barry, wakati Ghana ilifunga penalti zake kupitia kwa John Boye, Andre Ayew, Bertrand, Abdul Baba, Harrison Afful na Jonathan Mensah.

HISTORIA imejirudia. Ivory Coast imebeba ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2015) baada ya kuichapa Ghana kwa mikwaju ya penalti 9-8 katika fainali iliyofanyika mjini Bata, Guinea ya Ikweta usiku wa jana Jumapili.

Ivory Coast imeibuka kidedea kwenye fainali hizo kwa mikwaju hiyo ya penalti baada ya sare ya bila kufungana kufuatia mechi hiyo kuchezwa kwa dakika 120.

Matokeo hayo yanakumbusha fainali ya Afcon 1992, ambapo Ivory ilitwaa taji lake la kwanza la ubingwa wa Afrika kwa mikwaju ya penalti 11-10 baada ya sare ya bila kufungana kama ilivyotokea usiku wa jana.

Ushindi huo kwa Ivory Coast pia unamfanya Kocha Herve Renard kuweka rekodi ya kubeba ubingwa wa Afrika mara mbili ndani ya fainali tatu za karibuni, huku Avram Grant wa Ghana akizidi kuwa na mikwaju kwenye mikwaju ya penalti baada ya Ghana kuwa timu yake ya pili kuinoa kwa miaka ya karibuni na kupoteza kwa mikwaju ya penalti katika mechi za fainali.

Grant aliinoa Chelsea iliyofungwa kwa mikwaju ya penalti na Manchester United kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyofanyika mjini Moscow, Urusi mwaka 2008.

Kipa Boubacar Barry ndiye shujaa wa Ivory Coast baada ya kufunga penalti ya ushindi, huku pia akiwa ameokoa mikwaju miwili ya penalti ilikuwa na kipa mwenzake Brimah Razak.

Kwenye mikwaju huyo ya penalti ya fainali ya jana, Ghana ilifunga penalti zake mbili za kwanza zilizopigwa na Mubarak Wakaso na Jordan Ayew na kuwa na imani kwamba ingebeba ubingwa huo baada ya Ivory Coast kukosa mikwaju yake miwili ya kwanza iliyopigwa na Wilfried Bony na Gadji Tallo. Baada ya hapo kibao kilibadilika na Ghana walikosa penalti zao mbili zilizofuatia iliypigwa na Afriyie Acquah na Frank Acheampong na kuwafanya Ivory Coast kurudi mchezoni.

Mabingwa wapya wa Afrika, Ivory Coast walifunga penalti zao kupitia kwa Serge Aurier, Seydou Doumbia, Yaya Toure, Salomon Kalou, Kolo Toure, Kanon, Serey Die na Barry, wakati Ghana ilifunga penalti zake kupitia kwa John Boye, Andre Ayew, Bertrand, Abdul Baba, Harrison Afful na Jonathan Mensah.

Kabla ya mikwaju hiyo ya penalti, mechi hiyo iliyochezwa kwa dakika 120 ilishuhudia kosakosa nyingi zilizotokana na timu hizo kushambuliana kwa zamu huku, Ghana ikiwa imegongesha mwamba mara mbili katika dakika za kawaida.

Ivory Coast (4-4-2): Barry; Aurier, Bailly, K. Toure, Kanon; Gradel, Serey Die, Yaya Toure, Tiene; Bony, Gervinho.

Ghana (4-4-2): Brimah; Afful, Boye, Mensah, Baba; Atsu, Acquah, Mubarak, A. Ayew; Gyan, Appiah.