Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ivory Coast ilivyomalizana na Curacao

CURACAO Pict

Muktasari:

  • Pepe alifunga mabao mawili jana akiiwezesha Ivory Coast kufuzu hatua ya 32 bora baada ya ushindi muhimu dhidi ya Curacao.

PHILADELPHIA, MAREKANI: IVORY COAST wataingia katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia baada ya straika wa Villarreal, Nicolas Pepe kuibuka shujaa katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Curacao.

Pepe alifunga mabao mawili jana akiiwezesha Ivory Coast kufuzu hatua ya 32 bora baada ya ushindi muhimu dhidi ya Curacao.

Kikosi hicho cha kocha Emerse Fae kilihitaji sare tu kuhakikisha kinatinga katika nafasi mbili za juu kwenye Kundi E, lakini kiliweza kuchukua pointi zote tatu na kuiondoa Curacao ambayo ilimaliza bila ushindi wowote katika michuano yao ya kwanza ya Kombe la Dunia. Ivory Coast sasa watakutana na Ufaransa au Norway katika hatua ya 32 bora.

CURA 02

Pepe alihitaji dakika saba kufungua ukurasa wa mabao baada ya kutumia kosa la safu ya ulinzi ya Curacao. Pasi ya kurudi nyuma ya Jurien Gaari kwa Joshua Brenet ilidunda na kumfikia Yan Diomande, aliyetoa pasi ya mwisho ambayo Pepe aliimalizia kwa utulivu na kufunga.

Curacao walijibu vyema baada ya kufungwa na kuanza kuzuia mashambulizi ya Ivory Coast, ambapo krosi ya Diomande ilimkosa Amad Diallo ndani ya boksi, huku Leandro Bacuna akipiga shuti lililopita pembeni kabla ya mapumziko.

Franck Kessie aliona shuti lake likibadilishwa mwelekeo na kwenda nje kidogo ya lango, na upande wa pili Sherel Floranus alipiga shuti lililopita juu katika kipindi kilichojaa kasi mwanzoni mwa kipindi cha pili.

CURA 03

Hata hivyo, Ivory Coast walipata bao la pili dakika ya 64 kupitia Pepe, aliyepokea pasi sahihi ya Ibrahim Sangare ndani ya boksi na kufunga kwa shuti la kujipinda lililompita kipa Eloy Room ambaye hakuweza kurudia uokoaji wake wa awali dhidi ya Ecuador.

Curacao walijaribu kupunguza tofauti ya mabao, lakini shuti la Tahith Chong lilidhibitiwa kirahisi na kipa Yahia Fofana.

Ivory Coast walikaribia kuongeza bao la tatu mwishoni, lakini mguu wa Armando Obispo ulizuia krosi ya Bazoumana Toure kutoingia langoni.

Kwa mara ya kwanza Ivory Coast wamefanikiwa kushinda mechi mbili katika shindano moja la Kombe la Dunia wakichochewa na uchezaji bora wa Nicolas Pepe, waliishinda timu iliyokuwa nafasi 49 chini yao kwenye viwango vya Fifa.

CURA 01

Akiwa na miaka 31 na siku 27, Pepe alikuwa mchezaji wa pili mkongwe zaidi Afrika kufunga mabao mawili katika mechi ya Kombe la Dunia, baada ya Roger Milla (mara mbili akiwa na miaka 38 mwaka 1990).

Pia ni Muivory Coast wa pili mwenye zaidi ya miaka 30 kufunga katika michuano hiyo, baada ya Didier Drogba (miaka 32) dhidi ya Brazil 2010.

Bao la kwanza la Pepe liliandaliwa na Diomande, mchezaji kijana anayechipukia akiwa nyota wa kwanza mdogo Afrika kutoa pasi ya bao kwenye Kombe la Dunia tangu Rigobert Song na Marc-Vivien Foe 1994. Diomande pia ni mchezaji pekee katika karne hii aliyengeneza nafasi 10+ na kudribo mara 10+ katika mechi zake tatu za kwanza za Kombe la Dunia.

Kwa upande wa Curacao, safari yao ya kwanza ya Kombe la Dunia imeishia mapema, ambapo kikosi hicho cha Dick Advocaat kilijua ushindi ungeweza kukipeleka hatua ya mtoano kama moja ya timu bora za nafasi ya tatu, lakini kilishindwa kufanikisha hilo.

Kilishindwa pia kutisha sana katika lango la Ivory Coast, kikimaliza na takwimu mbovu za wastani wa 0.47 kutokana na mashuti 11, ambapo mawili pekee yalilenga lango. Ivory Coast walikuwa na wastani wa bao 1.3 kutokana na mashuti saba. Kwa ujumla, ilikuwa mechi iliyothibitisha ubora wa Pepe na uimara wa Ivory Coast, huku Curacao wakimaliza safari ya kwanza ya Kombe la Dunia bila ushindi.