Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya ubaguzi, Semenyo apendekeza adhabu

UBAGUZI Pict

Muktasari:

  • Semenyo alisema hilo baada ya kukabiliwa na maumivu makali ya kufanyiwa ubaguzi kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England wiki iliyopita.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Bournemouth, Antoine Semenyo amesema anaamini hukumu ya kifungo cha jela inaweza kuwa adhabu sahihi kabisa kwa wanaoendekeza ubaguzi wa rangi kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

Semenyo alisema hilo baada ya kukabiliwa na maumivu makali ya kufanyiwa ubaguzi kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England wiki iliyopita.

Wiki ya kwanza kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu England iligubikwa na tukio la mshambuliaji huyo wa Bournemouth kufanyiwa unyanyasaji wa kibaguzi na shabiki mmoja uwanjani Anfield, wakati timu hiyo ilipochapwa 4-2 na Liverpool.

Staa huyo wa kimataifa wa Ghana mzaliwa wa London, ambaye alifunga mara mbili kwenye mechi hiyo, alimwambia mwamuzi Anthony Taylor tukio la kubaguliwa kwa rangi yake huku shabiki huyo mwenye umri wa miaka 47 alikamatwa na polisi.

Mtu huyo alitolewa kwa dhamana, lakini aliadhibiwa kutohudhuria mechi yoyote huko England ikiwa ni moja ya masharti ya dhamana hiyo.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipofanyiwa ubaguzi, Semenyo aliiambia ITV News kunapaswa kuwa na adhabu kali ili kukomesha jambo hilo.

“Hii haikubaliki, haipaswi kabisa kutokea kwenye kipindi hiki na nyakati hizi. Adhabu inapaswa kuwa kali zaidi,” alisema.

“Inapaswa kuwa kifungo cha jela, inapaswa kufungiwa kwenda uwanjani kwa maisha yake yote na vitu vingine vya aina hiyo, lakini hali imekuwa vinginevyo. Nazungumzo kwa ajili ya wachezaji wote, kama jambo hilo litatokea, basi kuwe na adhabu kali.

“Hizi kampeni za kupinga ubaguzi zimekuwa zikiendelea kwa muda sasa, lakini kwa muda mrefu hainekani kuleta matunda. Naona kabisa kama kuna kitu kingine cha ziada kinapaswa kufanyika.”

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu England, Richard Masters alikazia kwenye jambo hilo baada ya kuiambia BBC Sport: “Hakuna mwanasoka wa Ligi Kuu England anapaswa kukutana na hii hali, iwe kwenye kazi yake au akiwa mapumziko, kukumbana na unyanyasaji huo.

“Hii inatufanya watu kama mimi na wengine wenye mamlaka kwenye mpira kufikiria mara mbili kitu kinachopaswa kutokea huko mbele. Kama ukikutwa na hatia kwamba umetumia lugha ambayo si nzuri, utaondolewa uwanjani, utafungiwa na tatu utafunguliwa kesi ya jinai.”

Semenyo, ambaye amewashukuru wachezaji wenzake, wachezaji wa timu pinzani na mashabiki kwa sapoti kubwa na kukemea matukio ya unyanyasaji kwenye kurasa zao kwenye mipango ya kijamii.