Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Son ipo hivi Spurs

SON Pict

Muktasari:

  • Son, 33, amedumu kwenye kikosi cha Spurs kwa muongo mmoja sasa na sasa timu hiyo imefungua milango ya kumpiga bei endapo itapokea ofa kati ya Pauni 15 milioni na Pauni 20 milioni. Na uhamisho wowote wa kwenda Marekani utazingatiwa kama mchezaji mwenyewe atakubali kwenda huko.

LONDON, ENGLAND: TOTTENHAM Hotspur inapiga hesabu za kukubali ofa ya Pauni 15 milioni kwa ajili ya kumpiga bei nahodha wao Son Heung-min baada ya staa huyo kuwindwa na miamba ya Marekani, LAFC.

Hata hivyo, Spurs itafanya uamuzi wa mwisho baada ya ziara yao ya pre-season huko Asia.

Son, 33, amedumu kwenye kikosi cha Spurs kwa muongo mmoja sasa na sasa timu hiyo imefungua milango ya kumpiga bei endapo itapokea ofa kati ya Pauni 15 milioni na Pauni 20 milioni. Na uhamisho wowote wa kwenda Marekani utazingatiwa kama mchezaji mwenyewe atakubali kwenda huko.

Son hataruhusiwa kuondoka kabla ya kwenda pre-season, ambapo mabingwa hao wa Europa League watakwenda kujipiga na Newcastle huko Seoul, Korea Kusini, Agosti 3. Na hilo litakuja baada ya mechi ya north London dhidi ya mahasimu wao Arsenal itakayopigwa Hong Kong.

Spurs kwenda Asia kunatokana na uwepo wa mchezaji Son kwenye kikosi chao, ambapo mchezaji huyo ni maarufu sana kwenye eneo hilo. Kutokana na hilo, Spurs, inaamini itapata hasara kubwa endapo kama itakwenda Korea Kusini bila ya huduma ya Son kwenye kikosi chao.

Yeye ni mchezaji muhimu kuwamo kwenye kikosi cha Spurs kulingana na mkataba wa kitalii uliosaini na klabu hiyo ya Ligi Kuu England kwa ajili ya kwenda kwenye nchi hiyo, endapo kama mchezaji hatakuwapo, Spurs itapoteza mapato iliyopaswa kuvuna kwenye dili hilo.

Staa huyo wa Korea Kusini, ambaye alishinda Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu England mwaka 2022, alionyesha kiwango bora pia msimu uliopita, alifunga mabao saba na kuasisti tisa katika mechi 30 alizocheza kwenye ligi.