Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya posho za wachezaji Super Eagles yamshangaza staa EPL

POSHO Pict

Muktasari:

  • Kikosi cha Super Eagles, juzi Jumanne, Novemba 11, 2025, kilisusia mazoezi ya mwisho kuelekea mechi ya mchujo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Gabon, itakayopigwa leo Alhamisi Novemba 13, 2025 katika Uwanja wa Moulay Hassan, mjini Rabat, Morocco.

Mchezaji wa zamani aliyetamba na klabu ya Watford katika Ligi Kuu ya England, Troy Deeney, ameshangazwa na kitendo cha wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, kususia mazoezi kwa shinikizo la kutaka walipwe posho zao kwanza.

Kikosi cha Super Eagles, juzi Jumanne, Novemba 11, 2025, kilisusia mazoezi ya mwisho kuelekea mechi ya mchujo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Gabon, itakayopigwa leo Alhamisi Novemba 13, 2025 katika Uwanja wa Moulay Hassan, mjini Rabat, Morocco.

Shinikizo hilo la wachezaji wa Super Eagles, lilielekezwa moja kwa moja kwa uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nigeria (NFF), ambao ulikuwa haujalipa posho hadi jana.

POS 02

Hata hivyo, jana Jumatano, Novemba 12, 2025 majira ya mchana, taarifa rasmi ilitolewa kutoka kambini, ikithibitisha kuwa matatizo yote yameshatatuliwa, na wachezaji wako katika hali nzuri ya kisaikolojia kuelekea mechi hiyo ya leo Alhamisi.

Deeney ameonyesha masikitiko yake kuhusu muda ambao matatizo kama haya yametokea, akibainisha kuwa si mara ya kwanza, ya pili, au ya tatu mambo ya nje ya uwanja kama haya kutokea katika nyakati muhimu kwa soka la Nigeria.

“Ni aibu ya kweli kwa sababu huu ni wakati mkubwa katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia, lakini sasa tena tunazungumza kuhusu mambo ya nje ya uwanja,” amesema Deeney katika mahojiano na CBS Sports Golazo.

POS 01

Endapo Nigeria itaifunga Gabon, itakutana na Cameroon au DR Congo katika mchezo wa kumsaka mshindi atakayecheza na mshindi wa mabara mengine ili kumpata mshiriki wa Kombe la Dunia 2026.

Cameroon itacheza dhidi ya DR Congo katika mechi nyingine itakayochezwa leo jioni.