Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya majeraha Arsenal yamtesa Arteta

Muktasari:

  • Arsenal ambao hadi jana, Jumamosi walikuwa wakiongoza ligi kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 73 kabla ya mchezo wao dhidi ya Fulham bado wapo kwenye mbio za makombe matatu, wamekumbwa na pigo la kukosa nyota wao muhimu hali iliyowafanya waonekane kuwa butu hasa katika safu yao ya ushambuliaji.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta ameonekana kuchoshwa na wimbi la majeruhi linaloikumba timu hiyo, hali iliyomlazimu kuchukua hatua nzito na kuamua kumpa kazi mtaalamu maalum kuchunguza tatizo hilo linalotishia kuvuruga mwenendo wao msimu huu.

Arsenal ambao hadi jana, Jumamosi walikuwa wakiongoza ligi kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 73 kabla ya mchezo wao dhidi ya Fulham bado wapo kwenye mbio za makombe matatu, wamekumbwa na pigo la kukosa nyota wao muhimu hali iliyowafanya waonekane kuwa butu hasa katika safu yao ya ushambuliaji.

Mastaa kama Martin Odegaard, Bukayo Saka na Kai Havertz wamekosa sehemu kubwa ya msimu kutokana na majeraha.

Takwimu zinaogopesha zaidi wachezaji wa Arsenal wamekosa jumla ya mechi 262 kwa klabu na timu za taifa msimu huu huku 141 kati ya hizo zikiwa ni ndani ya Ligi Kuu pekee.

Kwa kulinganisha, mabingwa watetezi Manchester City wamekosa mechi 135 pekee licha ya kuwa na kikosi kipana zaidi. Lakini kinachoumiza zaidi Arsenal ni kukosekana kwa mshambuliaji wao muhimu Havertz ambaye amecheza mechi chache sana huku nyota wa City Erling Haaland akikosa mchezo mmoja wa ligi.

Katika jitihada za kutafuta suluhisho, Arteta amemvuta rafiki yake wa karibu, mtaalamu wa tiba ya viungo kutoka Hispania, Joaquín Acedo, kusaidia kuchunguza chanzo cha tatizo hilo.

Acedo ana uhusiano wa karibu na Arteta na amewahi kufanya kazi na timu hiyo hapo awali huku akionekana mara kadhaa katika kituo cha mazoezi cha London Colney.

Licha ya kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tatu, Arsenal wako kwenye presha kubwa kwani Pep Guardiola na Manchester City wana mchezo mkononi hali inayoweza kubadili kabisa msimamo.

Mashabiki wa Arsenal wana hamu kubwa ya kumaliza ukame wa zaidi ya miaka 20 bila ubingwa wa ligi lakini wingu la majeruhi linaendelea kuwa tishio kubwa. Hali imezidi kuwa tete baada ya nahodha Odegaard kuonekana kupata maumivu katika mchezo dhidi ya Atletico Madrid huku Arteta akisema wanasubiri tathimini ya madaktari kujua hali yake.

Akizungumza kabla ya kuivaa Fulham, Arteta alikiri ukubwa wa tatizo hilo akisema: “Kai amekuwa pigo kubwa kwetu. Ni mmoja wa wachezaji muhimu sana katika safu ya ushambuliaji na amekosekana kwa muda mrefu.”